Mary Margwe, Simanjiro.
Mwekezaji Mzawa wa " Kitalu C " Onesmo Mbise wa Kampuni ya Franone Mining amemshuruku Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaamini wawekezaji wazawa juu ya uamuzi wake wa Mgodi wa Madini ya Tanzanite ' Kitalu C ' kupatiwa mwekezaji mzawa na Mtanzania
Hayo amebainisha jana wakati akizungumza na Watu wa makundi Maalum, ambapo watu wamakundi hayo Maalum walimualika Mkurugenzi huyo, Afisa Madini Mkazi Mirerani (RMO) Menard Msengi,na Msaidizi wake Ezra Gregory Ntaluka kwa lengo kumshukuru Mwekezaji huyo na viongozi hao Kwa kuwapatia zawadi kama Mbuzi ,blanketi, uku Mkurugenzi Mbise akipatwa Mbuzi blanketi, shuka la kimasai pamoja fimbo Maalum iliyoashiria alama na ushindi katika kuongoza kwenye eneo la Mgodi wa Kitalu C.
Mwekezaji Mbise amesema Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uamuzi sahihi juu ya Kitalu C kukabidhiwa Mwekezaji mzawa, kitendo ambacho naye ameahidi kujiaminisha kwake.
" Tunamshukuru sana mama yetu Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutuamini sisi wawekezaji wazawa, na sisi sasa hiki ndicho tunachowarudishia kwenu Mungu alichotujaalia" amesema Mbise.
Aidha awali Mbise amesema alipata mstuko baada ya kualikwa na akina mama hao na kukuta wameandaa mambo makubwa kuliko alivyofikiria, ambapo amewapongeza kwa kuonyesha Moyo wa shukrani kwao.
" Sasa Mimi mepata kama mstuko kidogo, sikujua kama mmeandaa jambo kubwa namna hii, lakini nipende kuwashukuru kwa jinsi mlivyojitoa kutupatia zawadi sisi sote hapa, kuwa na moyo wa shukrani ni jambo zuri sana unajua unamsaidia mtu wewe unaona ni kidogo lakini anarudisha shukrani inatia moyo wa kuendelea kumsaidia zaidi " amesema Mbise
Aidha nje ya hilo Mkurugenzi huyo aliombwa kuwa mlezi wa Kikundi Cha wazee jambo ambalo amelipokea huku akimtaka Katibu wa kikundi Anjela Mussa kuweza kupanga naonili aweze kuwapeleka Ofisini waone namna mkakati wao ulivyokaa, wajadili kuona namna ya kuwasaidia.
" Kuhusiana na suala la chakula kwa wazee tutakaa tuone uhitaji uliopo, na tukitoa tunaomba kiratibiwe vizuri, naona mnafanya kazi vizuri ila ila sasa Mazingira yenu ya kazi hapa kuna uhitaji mkubwa wa kujengewa choo hapa Mahali pa kazi ili kuweza kuweka Mazingira safi na salama, hivyo tuwawajenjea choo hapa" amesema Mbise.
Aidha aliwatahadhalisha viongozi wa makundi hayo Maalum kuhakikisha Vijana wenye nguvu hawaingii hapo Kwa wazee badala yake waende kufanya kazi zingine ili kazi hiyo waachiwe watu wa makundi maalum, vinginevyo hata kama watakua wakienda basi iwe mara moja moja n ask mfululizo.
"Mimi nawashukuru sana kwa yote, nadhani mmeona sasa udongo umeongezeka, na itaendelea kuongezewa kadri tutakavyojaaliwa na Mungu, nashukuru sana kwa kuendelea kudumisha amani na utulivu mahali pa kazi, naomba jitahidini sana kutunza Mazingira ili nayo yawatunze,msijenge vibanda kiholela hapa vinaharibu Mazingira, hakuna neno linguine dhidi ya kusema asante sana Kwa zawadi mlizo tubatia" ameongeza Mbise
Hata Mbise amesema walioajiriwa moja kwa moja na Kampuni ya Franone Mining ni watumishi 328, kati yao 30 ni Wataalam mbalimbali wanaohusika ndani ya uendeshaji wa Mgodi huo, waliobaki wote ni wafanyakazi wachimbaji
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...