Na John Walter-Babati

Makamu Mwenyekiti wa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) bara, Ndugu Abdulrahman Kinana amempongeza mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini Daniel Sillo kwa kazi kubwa ya kuwatumikia wananchi licha ya kuwa na majukumu mengi ya kibunge.

Kinana ametoa pongezi hizo Julai 24,2023 akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Ayalagaya wilaya ya Babati ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake katika mikoa mbalimbali nchini kukagua utekelezaji wa ilani ya chama cha Mapinduzi na kukiimarisha chama hicho.

Amewaambia wananchi wa Babati vijijni kuwa wamepata mbunge mchapa kazi ambaye ameaminika na wabunge wenzake na kuamua kumpa uwenyekiti wa kamati ya bajeti

"Huyo ambaye anataka kugombea jimbo la Babati vijijini anatafuta nini, anataka kufanya nini ambacho Sillo hawezi kufanya?" alihoji Kinana

“Kati ya wabunge wanaofanya kazi vizuri, Sillo ni mchapakazi na msikivu sana, mlifanya maamuzi sahihi kumchagua mbunge huyu naomba tumuunge mkono, watakaotaka kugombea ruksa, lakini ajiulize anataka kufanya nini ambacho Sillo hawezi"

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini Daniel Sillo amesema serikali imepeleka fedha nyingi kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo Kwa mwaka fedha 2022/2023 Halmashauri ilipokea Bilioni 4.1 kwa ajili ya kujenga vituo vya afya vinne pamoja na hospitali ya wilaya na vifaa tiba.
Sillo amesema kwa upande wa elimu, wamepokea Shilingi Bilioni 6.1 kwa ajili ya elimu ya msingi na Sekondari kwenye ujenzi wa Madarasa, Maabara na elimu bila malipo.

Kwa upande mwingine aliiomba serikali kuingilia kati migogoro iliyopo katika ya hifadhi na wananchi wanaoishi katika maeneo hayo na mivutano kati ya wawekezaji na wananchi ili kila mmoja afanye kazi za uzalishaji bila kuwa na kikwazo.

Ikumbukwe kuwa Mheshimiwa Daniel Sillo ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti na mwenyekiti wa Bunge.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...