Na Mwamvua Mwinyi,Pwani, Julai 25


MKUU wa Mkoa wa Pwani alhaj Abubakari Kunenge, ameeleza ni wajibu kwa kila mtu kushirikiana kulinda amani kwa kuwa sehemu ya kufichua vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani.

Ameeleza, kuna wakati zinatokea chokochoko kwenye maeneo yetu ni jukumu letu kwa pamoja kulinda ulinzi na usalama kwa kushirikiana na vyombo vya kisheria.

Kunenge alitoa rai hiyo kwenye kilele cha maadhimisho ya kumbukumbu ya mashujaa, yaliyofanyika kimkoa, katika mnara wa mashujaa uliopo viwanja vya Ofisi ya Mkoa wa Pwani Julai 25 mwaka huu.

Aidha alihimiza elimu ya historia ya mashujaa kutolewa kwa watoto na vijana kwa manufaa ya kizazi kijacho kuendelea kuthamini na kuienzi siku hii.

"Tuendelee kutoa taarifa za viashiria vya uvunjifu wa amani katika maeneo yetu,na kushirikisha kwa vyombo vyenye mamlaka ili kulinda utulivu uliopo '"

“Tunawapenda, kuwaenzi  viongozi wetu waliolipigania taifa letu, ni lazima kila mwananchi kutambua mchango uliofanywa na mashujaa katika kulipigania Taifa hili kwa kuhakikisha wanakuwa walinzi na kuripoti viashiria vya uvunjifu wa amani "alieleza Kunenge.

Kunenge alieleza, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jacob John Mkunda anafanya kazi kubwa kuhakikisha ulinzi na usalama wa wananchi, na amechukua nafasi hiyo kumpongeza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...