Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
Klabu za Tanzania zinazoshiriki Michuano ya Kimataifa, Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF CL) na Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC) zinatarajiwa kuanza kusaka mataji hayo msimu huu wa 2023-2024.
Katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa msimu huu, Tanzania inawakilishwa na Klabu za Yanga na Simba wakati kwenye Michuano ya Kombe la Shirikisho, Tanzania itawakilishwa na Azam FC na Singida Fountain Gate FC.
Mabingwa wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara msimu ulioisha, Yanga SC wataanza raundi ya awali ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa, wakicheza dhidi ya ASAS ya Djibouti huku wakisubiri mshindi wa jumla kati ya Association Sportive Otohô ya Congo au El Merreikh ya Sudan ili kucheza nao kwenye raundi ya kwanza.
Makamu Bingwa wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara msimu ulioisha, Simba SC wao wataanza raundi ya kwanza ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika wakisubiri mshindi wa jumla kati ya Africans Stars ya Namibia au Power Dynamos FC ya Zambia.
Matajiri wa Dar es Salaam, Azam FC watacheza dhidi ya Bahir Dar Kenema FC ya Ethiopia, kwenye raundi ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika, mshindi wa jumla katika mchezo huo atakutana na Club Africain ya Tunisia kwenye raundi ya kwanza ya Michuano hiyo.
Vile vile, kwenye Michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho Afrika, Singida Fountain Gate FC wataanza raundi ya awali dhidi ya majirani zao wa visiwani Zanzibar, JKU SC ambapo mshindi wa jumla atacheza dhidi ya Future FC ya Misri kwenye raundi ya kwanza ya Michuano hiyo.
Michezo yote kwa ujumla ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika itachezwa kati ya Agosti, Septemba na Oktoba mwaka huu kwa timu zote kucheza michezo hiyo nyumbani (home) na ugenini (away).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...