Na Rahma Khamisi Maelezo           25/7/2023

 

Wananchi wametakiwa kuvitumia  kwa usahihi vyandarua  watavyopewa serikali dhidi ya ugonjwa wa malaria  ili kujikinga na maambukizi ya mbu wa Malaria.

 

Akizungumza na Wananchi wa  Wilaya ya Mjini  katika hafla ya Uzinduzi wa Kampeni ya Ugawaji wa vyandarua vyenye dawa  huko Uwanja wa Matarumbeta, Waziri wa Afya Zanzibar Mhe, Nassor Ahmed Mazrui  amesema 

 

Amesema vyandarua  hivyo vyenye dawa vinadumu kwa muda  wa miaka 3na vinatolewa kwa  wananchi wote nchini.

 

Amesema vyandarua hivyo vitagawiwa kwa wote nchini vitasaidia kuzuwia maabukizi hivyo ni vyema kuvitumia kwa usahihi ili serikali ipate kufikia lengo la kutokomeza ugonjwa huo.

 

fedha hizo zimetumika kwa ajili ya kuwalinda  na kuwahifadhi wananchi dhidi ya mbu wa malaria.

 

 “Vyandarua hivi tunavitoa kwa matumizi ya binadamu na si vyenginevyo ,hivyo lazima tuvitumie katika njia sahihi  iliyokusudiwa ”, alifahamisha Waziri.

 

Amefahamisha kuwa  malaria bado yapo nchini  hivyo amewasisitza wananchi kujitahidi kuhifadhi mazingira  kwa kufanya usafi kila sehemu ili kujikinga kwani Mazingira machafu ndio yanapelekea mazalia ya mbu anaesababisha malaria.

 

Waziri Mazrui ameeleza kuwa jumla ya watu 3373 waliripotiwa kupata malaria na watu sita kufariki dunia  hivyo kutokana na hali hiyo Wizara inaswaisitiza wananchi kuendelea kutumia vyandarua watakavyopatiwa kwani kila mmoja ana jukumu la kutoa mchango wake kuondosha malaria .


“ Takwimu zinaonesha dhahiri kuwa malaria yapo Zanzibar  kwani kwa mwaka huu ugonjwa huo umesababisha vifo vya  watu sita tena vijana wadogo hii ni ishara mbaya na nidhahiri kuwa malaria hayajaondoka ,”Waziri aliwasisitiza wananchi.

 

Aidha Waziri ameongeza kuwa  asilimia 46 ya wakaazi ni kutoka Mkoa wa Mjini  hivyo  vyandarua  vitaanza kutolewa  katika Mkoa  huo ambao una wakaazi wengi wanaotoka maeneo tofauti .

 

Katika hatua nyengine Waziri amesema kuwa Serikali inapambana kuhakikisha wananchi wake wanapata afya bora, ni jukumu la kila mtu kutoa mchango wake ili Zanzibar ibaki salama kwani bila ya malaria inawezekana.

 

Waziri Nazrui amewataka wananchi kufuatilia terehe za ugawaji wa vyandarua na kufika vituoni mapema  kwa ajili ya kuchukua vyandarua vyao na kuvitumia kwa usahihi.

 

“Nawaomba wale waotoaji wa vibali vya ujenzi wa nyumba kuhakikisha wanatoa kwa kuzingatia maadili ya afya na  mazingira kwani nyumba nyingi zinayojenwa hazifuati masharti ya ujenzi na kupelekea kuwepo na mazingira hatarishi ma kupelekea mbu kuweka makaazi yao” alieleza Waziri Mzrui.

 

Akitoa taarifa kuhusiana na ongezeko la ugonjwa huo Meneja wa Kitengo cha kuzuwia  Malaria  Zanzibar  Shija Joseph Shija  amesema kuwa kuanzia January hadi June Wilaya ya Mjini na Wilaya ya Magharib “B” ndizo zinazoongoza ikifuatiwa na Wilaya ya kusini kwasababu ya  wananchi hao kuchelewa kufika hospitali mapema.

 

Ameeleza kuwa takwimu zinaonesha  wanaoathirika na ugonjwa huo zaidi ni vijana ,wanafunzi wasafiri na wanaofanya biashara ambao watembea maeneo tofauti.

 

Nae Mkuu wa Wilaya ya Mjini Rashid Msaraka   amewataka wananchi kutumia vyandarua hivyo kwa usahihi na kuvitunza kufikia leno lilikusudiwa la kutokomeza malaria nchini.

 

Amesema kuwa serikali imeanzisha mpango wa kufanya usafi kila  mwisho wa mwezi ili kutokomeza mazalia ya mbu yasienee katika jamii.

 

Nae  Muwakilishi kutoka Marekani ambae pia Naibu Mkuruenzi wa CDC  Anna Hothmen amewataka wananchi kuacha tabia ya  kutumia vyandarua katika shuhuli za uvuvi na kujengea bustani na badala yake kuvitumia katika matumizi sahihi ili kujikinga na maambukizi .

 

Zoezi la ugawaji wa vyandarua vilivyotiwa dawa linatarajiwa kuanza rasmi kesho tarehe 26 Julai mwaka katika Shehia 53 za Wilaya ya Mjini na limeandaliwa na Wizara ya Afya chini ya ufadhiliwa  wa Wadau mbalimbali wa Maendeleo wakiwemo USAD , CDC, GLOBALFOUND na BREAKTHROU ambapo jumla ya Tsh  430,o47zimetumika katika mradi huo.

Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui akitoa hotuba ya Uzinduzi wa Kampeni ya Ugawaji wa Vyandarua Vyenye Dawa kwenye Kaya,hafla iliofanyika Shehia ya Matarumbeta Wilaya ya Mjini Unguja.

Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui akimkabidhi Vyandarua Mkuu wa Kaya ya Matarumbeta ZONE "A"  katika  Uzinduzi wa Kampeni ya Ugawaji wa Vyandarua Vyenye Dawa kwenye Kaya,hafla iliofanyika Shehia ya Matarumbeta Wilaya ya Mjini Unguja.

Mkuu wa Wilaya ya Mjini Rashid Simai Msaraka akitoa salamu za Mkuu wa Mkoa katika hafla ya Uzinduzi wa Kampeni ya Ugawaji wa Vyandarua Vyenye Dawa kwenye Kaya,hafla iliofanyika Shehia ya Matarumbeta Wilaya ya Mjini Unguja.
Mkurugenzi Kinga Dk,Salim Slim akitoa hotuba ya Makaribisho katika Uzinduzi wa Kampeni ya Ugawaji wa Vyandarua Vyenye Dawa kwenye Kaya,hafla iliofanyika Shehia ya Matarumbeta Wilaya ya Mjini Unguja.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR,25-JULY-2023.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...