Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
Julai 26
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limewaasa madereva wanaoendesha Pikipiki (Bodaboda) na Bajaji kuwafichua watu wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu kwenye vijiwe vyao.
Akizungumza na madereva hao, leo Julai 26 kwenye ukumbi wa Benjamin Mkapa (Maisha Plus) ,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishina Msaidizi Pius Lutumo aliwataka waendesha Pikipiki (Bodaboda) hao kupiga simu wakati wowote kwake kumjuza watu wanaojihusisha na vitendo hivyo.
"Simu yangu ipo tayari kupokea taarifa zozote mlizo nazo zinazohusu vitendo vya kihalifu na nitazifanyia kazi ikiwa ni pamoja na kuwalinda wale watakaonipa taraifa).
Aidha, Kamanda Lutumo aliwataka Bodaboda hao kutoa taarifa za madereva wa mabasi, malori na magari madogo wanaokiuka kwa makusudi Sheria za usalama barabarani ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria na kupunguza matukio ya ajali za barabarani katika Mkoa wa Pwani.
"Ajali nyingi husababishwa na madereva kutokuheshimu Sheria hizo akitolea mfano ajali ya Basi la Saratoga iliyotokea usiku wa kuamkia Leo eneo la Tanita na kusababisha vifo kwa watu wawili akiwemo dereva wa basi hilo kutokana na uzembe wa dereva wa basi la Saratoga kuyapita magari mengine bila ya kuchukua tahadhari."
Kadhalika, Jeshi la Polisi limewapa nguvu viongozi wao kuweza kukamatana wao kwa wao kwa madereva wanaokiuka na kuvunja Sheria za usalama barabarani na yule atakae kaidi atakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani.
Takribani madereva 360 wa Pikipiki na Bajaji wa vijiwe vyote katika Wilaya ya Kibaha wameweza kupatiwa elimu kuhusu umuhimu wa uvaaji wa Kofia Ngumu, Haki na wajibu wa dereva awapo barabarani, udereva wa kujihami, kutojihusisha na uhalifu, kutobeba mishikaki, kutobeba mikaa, kuvaa viakisi mwanga vyenye utambuzi wa vijiwe vyao na kuheshimu na kuzingatia Sheria za usalama barabarani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...