Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
Julai 26
WATU wawili wamefariki Dunia pamoja na wengine watatu kujeruhiwa baada ya kutokea ajali , usiku wa kuamkia Julai 26 mwaka huu eneo la Tanita, kata ya Mkuza ,Kibaha Mkoani Pwani katika Barabara Kuu ya Dar es Salaam.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Pwani, Pius Lutumo alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo baada ya dereva wa bus la abiria lenye namba za usajili T.370 DHA aina ya Higer Kampuni ya Saratoga likiendeshwa na dereva Ammy Anuru likitokea Kigoma kuelekea Dar es Salaam kuyapita magari mengine pasipo kuchukua tafadhali na kugongana uso kwa uso na gari lililokuwa likitokea mbele yake.
"Bus hilo lilikuwa likitokea Mkoani Kigoma ambapo liligongana na gari lenye namba za usajili T.925 DRH lenye trela namba T.560 BLA aina ya HOWO Kampuni ya trans fuel likiendeshwa na dereva aitwae Hussein Hassan (37) mkazi wa Dar es Salaam lililokuwa likitokea Morogoro na kusababisha vifo hivyo"alifafanua Lutumo.
Lutumo alitaja waliopoteza maisha kuwa ni dereva wa bus la Saratoga Ammy Anuru mkazi wa Buguruni na abiria mmoja wa jinsia ya kiume bado hajafahamika jina lake anakadiriwa kuwa na miaka 20-25 .
Aidha majeruhi katika ajali hiyo ni Mnilu Mohammed (36) mkazi wa Ujiji Kigoma,Shaban Bomeka mkazi wa Kigoma (38) na Amani Jonathan mkazi wa Ilala Dar es Salaam.
Kamanda huyo alieleza kwamba, chanzo ni uzembe wa dereva wa bus la Saratoga kuyapita magari mengine pasipokichukua tafadhali na kugongana na gari lililokuwa mbele yake.
Majeruhi wa ajali wamelazwa hospital ya rufaa ya Tumbi mkoa wa Pwani kwa kufanyiwa matibabu zaidi.
Miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospital hiyo kwa uchunguzi wa daktari na itakabidhiwa kwa ndugu.
Lutumo aliwaasa, madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kujiepusha na ajali zembe.
Vilevile aliwataka abiria hasa wanaosafiri mikoa kujenga tabia ya kufichua madereva wasiofuata sheria za usalama barabarani na kwenda mwendo kasi sanjali na kushindwa kuchukua tahadhari.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...