Na Mwandishi Wetu,Zanzibar
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kwa kushirikiana na Marekani imezindua kampeni ya ugawaji wa vyandarua vyenye dawa yenye kaulimbiu "Usingizi Bul Bul Usiku wa Amani".
Kampeni hiyo inakusudia kusambaza vyandarua vyenye dawa takriban 248,000 katika shehia 53 za Unguja, visiwani humo.
Hatua inalenga kuongeza Kasi ya mapambano dhidi ya malaria na kwamba shehia zitakazosalia zitapokea vyandarua mwaka 2024.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa ugawaji wa vyandarua hivyo leo Julai 25, 223, Waziri wa Afya wa Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui alisema, hatua hiyo inathibitisha nia ya SMZ kutokomeza malaria Zanzibar.
"Kampeni hii inaonyesha nia yetu Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushikiana na Mpango wa Rais wa Marekani wa kupambana na Malaria (PMI) katika kutumia mfumo wa kidigitali kuboresha huduma za usajili na ugawaji wa vyandarua vyenye dawa katika kaya.
"Tunatoa shukrani zetu kwa USAID, PMI na washirika wote kwa mchango wao usioelezeka. Kwa pamoja, tuna imani kuwa juhudi hizi za pamoja zitatupeleka kufikia malengo ya Zanzibar isiyo na Malaria.
"Kwa mara ya kwanza hapa Zanzibar, mfumo wa kidigitali wa usajili na utoaji wa vyandarua umewasilishwa kusaidia wananchi kufanya usajili wa kaya zao, kupokea vyandarua kwa urahisi na kupunguza kadhia za kusubiri foleni ili kupata huduma," alisema.
Aidha, Mradi wa Digital Square, unaofadhiliwa na USAID, kwa kushikiana na ZAMEP wametengeneza mfumo wa kidigitali unaorahisisha usajili na ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kupunguza kucheleweshwa kwa usambazaji na kuhakikisha kuwa wananchi wengi wananufaika na vyandarua hivyo.
"Kupitia kampeni ya Usingizi Bul Bul inayotekelezwa wakati wa usajili na ugawaji wa vyandarua katika jamii inadhihirisha dhamira ya Serikali na nchi kwa ujumla kutokomeza malaria Zanzibar," amesema Anna Hoffman, Kaimu Mkurugenzi wa Ofisi ya Afya ya USAID Tanzania.
Ameongeza kuwa "Marekani itaendelea kutoa kushikiana na serikali ya Zanzibar katika jitihada za kutekeleza hatua mbalimbali zinazolenga kutokomeza malaria."
Amesema kupitia uzinduzi huo wanawahimiza Wazanzibari kuvipokea vyandarua hivyo na kuvitumia kwa kulalia kila siku.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...