Na Mwandishi Wetu.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema katika Mtaala wa Elimu unaondaliwa, Sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imepewa kipaumbele ili Watanzania waweze kuongeza utaalamu katika vipaji walivyonavyo
Mhe. Chana amesema hayo Julai 2, 2023 katika ziara ya Sekondari Iwawa iliyopo wilayani Makete mkoani Njombe.
"Sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo inapewa kipaumbele, kwa kuwa sio tu inachangia katika Pato la Taifa, pia imekuwa ni Sekta inayoajiri na kutoa furaha kwa jamii. Serikali iaendelea kuweka mazingira mazuri ikiwemo kutoa mikopo kupitia Mfuko wa Utamaduni na Sanaa pamoja na Mfuko wa Maendeleo ya Michezo ili kukuza sekta hizi, amesema Mhe. Chana
Ameongeza kuwa katika mwaka huu wa fedha, Wizara itatekeleza Programu ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Mtaa kwa Mtaa ambapo amesisitiza jamii kutobadilisha matumizi na badala yake kuyalinda maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya michezo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...