Kutoka kushoto mwenye suti nyeusi ni Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mheshimiwa Nickson Simon akisalimiana na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Wilaya ya Kibaha (UWT) Mwalimu Mwajuma Nyamka wakati akiingia kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Mji Kibaha.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mussa Ndomba akisoma waraka huo.
Na Khadija Kalili Michuzi Tv
MWENYEKITI wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mussa Ndomba amemuomba Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kuipandisha hadhi Halmauri ya Mji Kibaha na Kuwa Manispaa kwa sawababu imekidhi sifa na vigezo kwa asilimia 78 kuwa Manispaa.
"Nasema haya kwa sababu Mkoa wa Pwani ni kati ya Mikoa mikongwe ambao umeasisiwa 1975 hivyo hata Halmashauri ya Mji Kibaha ni Kongwe ambayo pia ni Makao Makuu ya Wilaya zote ndani ya Mkoa wa Pwani hivyo tunamuobma Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan atupandishe hadhi na kuwa Manispaa kwani jambo hili limeshazungumzwa sana katika mikutano mbalimbali ya Siasa nchini kadhalika Mbunge wetu wa Jimbo la Kibaha Mjini Mheshimiwa Silyvestery Koka amelisemea sana akiwa katika vikao vya Bunge Jijini Dodoma pia niwakumbushe ndugu wajumbe hata kwenye kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 jambo hili limezungumziwa kwenye majukwa ya siasa" amesema Ndomba.
Wakati huohuo Mwenyekiti huyo amesema kuwa kwa niaba ya Madiwani na viongozi wa Halmashauri Kibaha anamuomba Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kutoa idhini ya kumegewa eneo la Shirika la Elimu Kibaha kwa ukubwa wa ekari 576 lililopo kandokando ya barabara iendayo Morogoro ikiwa ni katika kuweka mandhari nzuri na ya kuvutia ya Halmashauri ya Mji Kibaha iliyopo Mkoani Pwani kwa wanaoingia na kutoka.
"Mheshimiwa Rais tunamuomba atupatie eneo la ukubwa wa hekari 576 ili Halmashauri iweze kuweka mipango miji mizuri ikiwemo uwekezaji kwa wafanyabiashara na kuuweka mji katika hali ya kuvutia pindi unapoingia, Kibaha ni Wilaya mama na lango la kuingia Mji wa mkubwa wa biashara Dar es Salaam tofauti na ilivyo hivi sasa kwani hakuna mandhari nzuri kwa sababu ya kuonekana mapori tu ambayo kwa sasa ni eneo linalomilikiwa na Shirika la Elimu Kibaha lenye ukubwa wa hekari zaidi ya 3000 ambazo wahusika wameziacha zikiwa mapori bila ya kufanya jitihada zozote za kuendeleza katika eneo hilo"amesema Ndomba.
Amesema kuwa endapo Halmashauri ya Mji Kibaha itapatiwa eneo hilo la ukubwa wa hekari 576 tu watapanga shughuli za maendeleo ya Mji Kibaha.
Mwenyekiti Ndomba amesema hayo katika kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya nne ya mwaka kilichofanyika mwishoni mwa wiki na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka vya ma vya siasa , wakuu wa Idara zote na wataalamu ndani ya Halmashauri hiyo akiwamo Mkuu wa Wilaya Kibaha Nickson Simon, Mkurugenzi Mhandisi Mshamu Ali Munde pamoja na wananchi wa Wilayani hapa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...