Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja leo Julai 11, 2023 ametembelea banda la Wizara ya Maliasili kujionea shughuli zinazofanywa na Taasisi mbalimbali zilizo chini ya Wizara yake katika maonesho ya 47 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea Jijini Dar es Salaam na kuipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Kwa kuendeleza Utalii wa Malikale
Pongezi hizo zimeelekezwa Kwa Taasisi hiyo Kwa jitihada za dhati katika kuboresha miundombinu ya Utalii katika maeneo hayo, Kwa kununua boti la Kisasa linalotoa huduma Kwa watalii wanaotembelea hifadhi ya magofu ya kale ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara
Sanjari na uboreshaji wa miundombinu katika hifadhi hiyo, Mhe. Mary Masanja pia ameipongeza TAWA Kwa kazi nzuri ya kuhamasisha watanzania kutembelea hifadhi hiyo ambapo watalii wengi wa ndani wameonekana wakifanya safari nyingi za Utalii katika hifadhi hiyo.
Pia Mhe. Mary ameipongeza TAWA Kwa kuunganisha Utalii wa malikale, Wanyamapori na bahari kitu ambacho kinatoa wigo mpana Kwa watalii kufanya shughuli zao za Kitalii katika maeneo mbalimbali yenye vionjo tofauti vya Utalii ambapo Kwa kufanya hivyo watalii wanaongeza idadi ya siku za kukaa katika Nchi Yetu na hivyo kuongeza kipato.
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...