Na Mathias Canal, Moshi-Kilimanjaro

Mbunge wa Viti maalumu Mhe Ummy Nderiananga ambaye pia ni Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) akiwa katika ziara mkoani Kilimanjaro amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa imani kubwa aliyompatia ya kumteua kuwa Naibu Waziri.

Akizungumza Katika mkutano na wananchi uliofanyika katika kijijini kwao Lotima ambapo ndipo alipozaliwa katika Kata ya Makuyuni ambapo ameeleza umuhimu wa shule za kata katika kuimarisha elimu nchini kwani zimeongeza chachu ya mafanikio kwa wananchi ambapo ametolea mfano yeye ambaye alisoma katika shule hizo.

Amesema kuwa Rais anafanya kazi usiku na mchana hivyo watanzania wanapaswa kumtia moyo na kumuunga mkono ili aweze kufikia dhamira ya kuwaletea maendeleo endelevu.

"Mhe Rais Samia ana upendo mkubwa na wana Kilimanjaro na sisi wanamakuyuni tumeona upendo wake, tumeona kujali kwake na kuthamini kwake" Amekaririwa Mhe Nderiananga

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Vunjo Mhe Dkt Charles Kimei amemshukuru Rais Samia kwa kuendelea kuboresha huduma mbalimbali za maendeleo ikiwemo utengenezaji wa barabara ya Himo-Makuyuni kwa kiwango cha lami ambayo imeshaanza kutengenezwa.

Amesema kuwa ujenzi wa barabara hiyo utarahisisha huduma za kijamii ikiwemo usafirishaji wa mazao ya chakula na biashara.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mhe Kisare Makori ameshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan Kwa miradi mingi ya maendeleo katika Wilaya ya Moshi.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...