Shazia Shafi, binti wai Kitanzania mwenye umri wa miaka 12. Amezaliwa nchini Uingereza katika mji wa Reading na kuhamia Jiji la Abu Dhabi nchi za falme za Kiarabu akiwa na umri wa miaka miwili pamoja na wazazi wake Dkt Shafi Ayoub Mohammed na Bi Aziza Mohammed Saleh.

Shazia ni binti wa kwanza wa kitanzania mwenye umri mdogo kuandika kitabu kwa lugha ya kiingereza chenye kurasa zaidi ya mia . Alianza kuandika kitabu hiki akiwa na umri wa miaka 9 na kukikamilisha akiwa na umri wa miaka 10.

Kitabu hiki kinaitwa "REBORN", maana yake KUZALIWA TENA. 

Kitabu kina kurasa zaidi ya mia. Kitabu kinahusu kisa cha msichana  aitwae Kate.

Hapo mwanzo msichana huyu alikuwa katika familia ya kimasikini.Hali ya familia ikabadilika kiuchumi msichana huyu alipofika umri wa miaka 7. 

Mabadaliko haya yalimfanya msichana huyu kubadilika kitabia na muonekano katika jamii.

Msichana huyo alipata ajali ambayo  ni sababu ya kuleta mabadiliko katika maisha yake. Na hii ndio  sababu ya kitabu hiki kuitwa REBORN au KUZALIWA TENA.

Upatikanaji wa Kitabu

Kitabu hiki kinapatikana kwa hard copy katika tovutiza AMAZON na Publisher  AUSTIN MCKAULEY. 

Unaweza pia kununua copy ya electronic ya kitabu hiki kwa ku download kwa kindle kutoka ktk tovuti ya AMAZON.

Kwa  hapa Tanzania, kitabu hiki kinaweza kupatikana kutoka  Elite Book Store iliyopo pale Mbezi Beach maeneo ya Tangi Bovu.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...