Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi ameondoka nchini baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali kuhusu Rasilimali Watu (Africa Human Capital Heads of State Summit) uliofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 25 na 26 Julai, 2023.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam , Mhe. Rais Nyusi amesindikizwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.), Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila na Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, mhe. Faustine Kasike.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...