Na Immaculate Makilika - MAELEZO

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Bara la Afrika linahitaji mageuzi katika nyanja zote muhimu kwa ajili ya maendeleo ya bara hilo.

 

Kauli hiyo ameitoa leo wakati akihutubia katika kilele cha mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu uliofanyika Jijini Dar es Salaam.

 

“Ni wazi kuwa Bara letu bado linahitaji mageuzi makubwa katika nyanja zote muhimu za uzalishaji na maendeleo. Na haya ndio malengo na madhumuni ya ajenda ya Maendeleo ya Afrika tunayoitaka ya mwaka 2063 ambayo imeweka malengo 7”, alieleza Mhe. Rais Samia.

 

Mhe. Rais Samia alisisitiza “Nataka nijielekeze kuyazungumzia malengo manne, ambayo ni  Afrika ambayo mafanikio yake yanajikita kwenye ukuaji jumuishi wa uchumi na maendeleo endelevu,  Bara lenye utangamano kisiasa kwa kuzingatia fikra za kimajumuishi na mwelekeo wa kimapinduzi,  Afrika inayozingatia misingi ya utawala bora, demokrasia, haki za binadamu na utawala wa sheria na  Afrika ambayo maendeleo yake yanatokana na watu kwa kutumia vipaji vyao, hususan wanawake na vijana pamoja na kutoa makuzi bora kwa watoto”.

 

Zaidi ya watu 1,200 kutoka nchi mbalimbali za Afrika wakiwemo Wakuu wa Nchi hizo, viongozi wa Serikali, Watumishi wa Umma, wadau, Waandishi wa Habari pamoja na wananchi wameshiriki Mkutano huo wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu  ulioanza  Julai 25, 2023 na kumalizika Julai 26, 2023.

 

Mbali na masuala ya rasilimali watu hususan kwa vijana, mkutano huo ulizungumzia pia sekta ya elimu, afya, kilimo, fedha na sayansi na teknolojia ambapo zimejadiliwa kama wazalishaji wa rasilimali watu.

 


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...