Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi pamoja na Wananchi wa Malawi kwenye maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Nchi hiyo kwenye Sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Taifa wa Bingu, Lilongwe nchini humo tarehe 6 Julai, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na Mwenyeji wake Rais wa Malawi Mhe. Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera wakati Gwaride la Heshima likipita mbele ya Jukwaa Kuu katika maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Malawi yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa wa Bingu, Lilongwe nchini humo tarehe 6 Julai, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akicheza ngoma pamoja na kikundi kimoja cha ngoma za asili kutoka Malawi wakati wa maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Malawi kwenye Sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Taifa wa Bingu Mutharika, Lilongwe nchini humo tarehe 6 Julai, 2023.

Vikundi mbalimbali vya ngoma za asili kutoka Malawi vikitumbuiza kwenye maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Malawi kwenye Sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Taifa wa Bingu, Lilongwe nchini humo tarehe 6 Julai, 2023.

Shamra shamra za maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Malawi kwenye Sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Taifa wa Bingu, Lilongwe nchini humo tarehe 6 Julai, 2023.

Rais wa Malawi Mhe. Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera akiwa pamoja na viongozi wengine wakicheza ngoma za asili wakati wa maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Malawi kwenye Sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Taifa wa Bingu, Lilongwe nchini humo tarehe 6 Julai, 2023.

Wageni mbalimbali waliohudhuria maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Malawi kwenye Sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Taifa wa Bingu Lilongwe nchini humo tarehe 6 Julai, 2023.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...