TAASISI ya Elimu Tanzania (TET) imewakaribisha wadau mbalimbali kutembelea banda la TET siku ya Maadhimisho ya Sabasaba katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam kwenye viwanja vya TanTrade Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika Maonesho hayo leo Julai 6,2023 Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu na Utawala TET, Bw.Moses Ziota amesema wananchi wakipata fursa kutembela banda hilo wataweza kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu TET pamoja na kujipatia vitabu vya kiada kwa shule za msingi na sekondari.
Amesema wamekuwa na vitabu vya aina mbalimbali pamoja na machapisho ambayo kwa kawaidia yanasaidia kumuwezesha mwanafunzi kupata maarifa .
Aidha amesema kuwa TET wamekuwa wakishiriki Maonesho hayo mara kwa mara kitu ambachi kimechangia ongezeko kubwa la wadau kujitokeza kutembelea banda hilo kwenye Maonesho ya mwaka huu.
"Taasisi yetu imekuwa ikijishughulisha na uandaaji wa machapisho mbalimbali na vitabu vya kiada kwaajili ya wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari, hivyo katika Maonesho haya Wadau tunawakaribisha ili waje wajifunza mambo mbalimbali yanayohusu TET".
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...