Na. Damian Kunambi, Njombe

Imeelezwa kuwa wananchi wa kijiji cha Ndowa kilichopo katika kata ya Makonde wilayani Ludewa mkoani Njombe ndani ya mwezi mmoja ujao wanakwenda kuondokana na changamoto ya upatikanaji huduma ya afya na kuwaondoa katika adha ya kutembea umbali wa zaidi ya km. 250 wanayo kabiliana nayo kwa miaka mingi hadi hivi sasa katika kufuata huduma hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na Mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya hiyo Stanley Mlay kwa njia ya simu mara baada ya mbunge wa jimbo hilo Joseph Kamonga kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi hao alipokuwa katika mkutano wa hadhara katika kijiji hicho kitongoji cha Liunji ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa halmashauri hiyo kupitia mapato yake ya ndani tayari ilitoa fedha kiasi cha sh. Mil. 34 toka mwezi Aprili hivyo ameshangazwa kuona fedha hizo kuendelea kusalia kwenye akaunti badala ya kufanya kazi iliyo kusudiwa na kuhitaji ufafanuzi zaidi juu ya fedha hizo kutoka kwa mganga mkuu huyo.

Mganga mkuu huyo alikiri kuingizwa kwa fedha hizo na kuongeza kuwa kwa sasa ujenzi utaendelea na unatakiwa kukamilika kwa kipindi cha mwezi mmoja ambapo mpaka sasa tayari vifaa tiba vimekwisha wasili wilayani kwaajili ya zahanati hiyo na watumishi wawili wamekwisha andaliwa hivyo aliwataka wananchi kuungana na serikali katika shughuli ndogo ndogo za ukamilishwaji wa zahanati hiyo ili iweze kuanza kutoa huduma baada ya mwezi huo mmoja.

"Kila kitu kipo tayari kwaajili ya ukamilishwaji na utoaji huduma ya zahanati hiyo hivyo wananchi tuungane kwa pamoja katika kuchangia nguvu kazi ili nanyi muweze kunufaika na hii hudumaya afya", amesema Dkt. Mlay.

Hata hivyo kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho amekiri kuziona fedha hizo kwenye akaunti ya kijiji na kusema kuwa alikuwa akisubiri maelekezo na mwongozo juu ya matumizi ya fedha huzo.

Aidha mbunge wa jimbo hilo alionekana kukasirishwa na ucheleweshaji wa umaliziaji wa zahanati hiyo kwani fedha hizo ziliingizwa takribani miezi mitatu iliyopita hivyo haiwezekani kukaa kwa muda wote huo kwa madai ya kuwa ya kusubiri mwongozo.

" Huu ni uzembe wa hali ya juu na usio kubalika, haiwezekani wananchi waendelee kupata tabu ya kutembea kwa miguu umbali mrefu kufuata huduma wakati tayari utatuzi wa changamoto yao upo, wananchi hawa wanako fuata hiyo huduma kwa mwendo wa gari tuu ni mbali je vipi kwa hawa wanaotembea kwa miguu?", Amesema Kamonga.

Zahanati hiyo mpaka hatua hiyo iliyofikiwa imechangiwa na wananchi hao kiasi cha zaidi ya sh. Mil 20 huku mfuko wa jimbo ikitoa kiasi cha sh. Mil. 1.59 na halmashauri ya wilaya hiyo awali ikitoa kiasi cha sh. Laki 2.





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...