Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,akizungumza na Bodi ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) pamoja na watumishi jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo,akizungumza na Bodi ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) pamoja na watumishi jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Prof. Michael Ng,umbi,akizungumza mara baada ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda kuzungumza na bodi hiyo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Dkt.Naomi Katunzi,akizungumza mara baada ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda kuzungumza na bodi hiyo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,aakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzungumza na Bodi ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) pamoja na watumishi jijini Dar es Salaam.
Na.Mwandishi Wetu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ameitaka Bodi ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) kujipanga katika kuhakikisha hairudufu kazi za taasisi nyingine na kuhakikisha wanachokifanya kinatimiza kiu ya watu wanaotaka kusoma elimu bila kikomo.
Prof. Mkenda amesema hayo Jijini Dar es Salaam wakati alipofika katika Taasisi hiyo na kuzungumza na Bodi pamoja na watumishi ambapo amesisitiza kuwa fursa za kusoma lazima zipatikane katika maisha yote ya binadamu hivyo ili kuendana na mabadiliko mbalimbali inapaswa kuangalia upya majukumu ya taasisi hiyo.
Kiongozi huyo pia amewataka kukaa na kushirikiana na wadau mbalimbali wenye uzoefu na uelewa wa kutosha juu ya elimu bila kikomo ili kuangalia ni mambo gani yanapaswa kuongezwa ama kupunguzwa katika majukumu yake ili kuwa na ufanisi na tija katika matumizi ya serikali
“Kuna Taasisi nyingi ambazo zinatoa elimu bila kikomo za serikali kama Chuo Kikuu Huria na Taasisi nyingine za binafsi hivyo ni muhimu kwa bodi na taasisi kuangalia upya majukumu yenu ili msifanye vshughuli ambazo zinafanywa pia na taasisi nyingine” ameongeza Prof. Mkenda
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amesema Taasisi hiyo inafanya kazi nzuri lakini baada ya matokeo ya sensa yameonyesha kuna asilimia kubwa ya watanzania ambao bado hawana ujuzi wa kusoma na kuandika vizuri hivyo ni kazi ya taasisi hiyo kuhakikisha watanzania wanakuwa na ujuzi wa msingi wa kusoma na kuandika.
Prof. Nombo ameongeza kuwa katika kutatua changamoto hiyo ya watu kutokujua kusoma na kuandika kupitia miradi na programu za taasisi hiyo zinawezesha kupunguza idadi ya watanzania wasiojua kusoma na kuandika, kwani haiwezekani kufanya maendeleo yeyote bila ya kuwa na ujuzi wa kawaida wa kusoma na kuandika.
“Juzi Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alihitimisha kilele cha mkutano wa viongozi wa Afrika juu ya rasilimali watu ambo ni hawa hawa Watanzania ambao tunaona kuanzia motto mpaka mzee, kwa hiyo hawa wote wanapaswa wapate ujuzi wa kusoma na kuandika hivyo wale walingwa wa taasisi yetu lazima tuhakikishe tunawatendea haki kwa kuwapa stadi hizo” amesisitiza Prof. Nombo
Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Prof. Michael Ng,umbi amemwambia Waziri huyo kuwa katika kipindi cha miaka mitatu wizara iliwapatia shiling bilioni 9.4 kutoka katika Mradi wa SEQUIP kwa ajili ya kuboresha mfumo wa elimu ya sekondari kwa njia mbadala kwa kuhuisha mihtasari, kuandaa miongozo, kuandika na kuchapisha moduli pamoja na kuwaandaa na kumotisha walimu.
Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa mbali ya shughuli za kuboresha mfumo wa sekondari na kuandaa walimu pia fedha hizo zimetumika kuimarisha mbiundombinu katika mikoa minane ya Pwani, Rukwa, NManyara, Iringa Mtwara, Kigoma na Singida na ukarabati mkubwa katika mikoa ya Morogoro, Ruvuma, Kilimanjaro, Dar es Salaam na Tabora.
Aidha Prof. Ngu’umbi amesema wadau wengine wamechangia shilingi bilioni moja kwa ajili ya utekelezaji wa Mpango wa Elimu Changamani kwa Vijana walio Nje ya Shule (IPOSA), Mpango wa Elimu Changamani baada ya Msingi (IPPE) na uboreshaji wa Mpango wa Mukeja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...