Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
BAADA ya kutangaza kuwauzia Azam FC Kiungo Mkabaji, Yannick Bangala Litombo, Wananchi Young Africans SC wametangaza kumsajili Mshambuliaji raia wa Ghana, Hafiz Konkoni kutoka Klabu ya Bechem ya nchini humo.
Konkoni pia amewahi kucheza Klabu za Bolga All Stars. Yanga SC wametangaza usajili wa Mshambuliaji huyo ambaye atasaidiana na kina Kennedy Musonda na Clement Mzize, Crispin Ngushi ambao wapo Kikosini badaa ya kuondoka kina Fiston Mayele.
Wachezaji wa kigeni waliosajiliwa Yanga SC nsimu huu ni Mahlatse Makudubela (Skudu) kutoka Afrika Kusini, raia wa Ivory Coast, PacĂ´me Zouzoua, Kouassi Attohoula Yao, Gift Fred kutoka Uganda na Maxi Mpia Nzengeli kutoka DR Congo. Wachezaji wa ndani (Tanzania) ni Jonas Mkude na Nickson Kibabage.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...