Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) ameiagiza Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kuweka kambi Mkoani Arusha kwa lengo la kurasimisha wafanyabiashara wa kilimo ili wapate leseni, tini na vibali vya kusafirisha mazao nje ya nchi.
Dkt. Kijaji ameyasema hayo Agosti 1, 2023 alipokutana na wafanyabiashara wa Mkoa wa Arusha kwa lengo la kusikiliza changamoto walizonazo na kuzitatua
Aidha, Dkt Kijaji amewaonya wafanyabiashara wazawa kuacha mara moja tabia ya kukata leseni na kuwauzia wageni wanaokuja nchini kununua mazao hadi mashambani badala ya kuyafuata kwenye masoko husika
Amesema endapo wafanyabiashara wa mazao wakirasimishwa na kupata leseni zao wataweza kutambulika, idadi yao itajulikana ili kurahisisha jitihada za kuwakwamua kiuchumi wafanyabiashara na wakulima wanauza mazao ya nafaka mbalimbali nchini.
Waziri Kijaji pia amebainisha kuwa Serikali iko mbioni kufuta vibali vya usafirishaji wa mazao vinavyokatwa kila mkoa badala yake kibali kiwe kimoja tu kilicholipiwa kila kitu ili kuwezesha wafanyabiashara wa mazao kubeba mizigo yao na kupelekea mahali husika bila kukata vibali kila Mkoa wanapopita.
Awali Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wadogo(Machinga) Bi. Amina Samson Njoka akiongea mbele ya Waziri Kijaji amesema wafanyabiashara wadogo katika jiji hilo wamekuwa wakilalamika kuhusu tozo nyingi kutoka OSHA, Jeshi la Zimamoto, Idara ya Uhamiaji pamoja na Halimashauri ambazo zimekuwa kero na kuomba kiwa tozo hizo zitizwe zote mara moja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...