Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt Ashatu Kijaji (Mb.) awataka Maafisa Biashara wote nchini kukagua bei ya Sukari duka kwa duka na atakae kutwa na bei zaidi ya shilingi 3,200 achukuliwe hatua za kisheria.

Waziri Kijaji ameyasema hayo Agosti 2, 2023 alipotembelea Kiwanda cha kuzalisha Sukari cha TPC Mkoani Kilimanjaro kujionea shughuli za uzalishaji na kisikiliza changamoto walizonazo.

Dkt. Kijaji  amesema ni jukumu la Maafisa  Biashara kutambua mfanyabiashara yeyote atakayeuza sukari juu ya bei kati ya 2800 na 3200 kumchukulia hatua.

Dkt. Kijaji amesisitiza kiwa  ni jukumu  la Serikali kulinda bidhaa yoyote inayotengenezwa nchini na kufanya Juhudi  za kila namna ili kuweza kuwasaidia wawekezaji na wafanyabiashara kuwa na  mazingira bora na wezeshi  ili kukuza biashara zao na kiwa na tija. 

Aidha, amesema bidhaa zinazotengenezwa nchinj zinatakiwa kuwanufaisha wawekezaji na wafanyabiashara wa ndani na biashara yoyotee inayofanyika nje ya nchi inatakiwa kuwa rasmi.

Vilevile amekipongeza Kiwanda  cha kuzalisha Sukari cha TPC kwa kutoa ajira zaidi ya elfu 3200 na jinsi kinavojihusisha na utoaji wa huduma kwa jamii inayokizunguka 

Naye Kaimu Afisa Mtendaji Utawala wa Kiwanda cha TPC, David Shiltu amesihi watanzania kuwa na Amani kwa kuwa sukari ipo sokoni ya kutosha na hakuna uhaba na uzalishaji unaendelea.










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...