Na Mwandishi wetu, Ruangwa.

JESHI la Zimamoto na Uokoaji limewataka wananchi kuwa na vifaa vya kuzimia moto wa awali ili kuokoa maisha ya watu pamoja na kuzuia uharibufu mkubwa wa mali zao hata kabla Jeshi hilo halijafika katika eneo la tukuo.
Hayo yamesemwa na Stesheni Sajenti Enock Mapunda wa Jeshi la Zimamoto na Ukoaji mkoa wa Lindi wakati wa maonyesho ya madini na fursa za uwekezaji yanayoendelea mjini Ruangwa.

“Lengo la kukabiliana na moto wa awali ni kusaidia Jeshi la Zimamoto na Ukoaji kuuzima moto na pia kusaidia mali na maisha ya wananchi kuwa katika hali ya usalama,” amesema Mapunda.

Aidha amesema, jeshi hilo limejipanga kutoa elimu kwa jamii hususan wachimba madini jinsi ya kuweza kuwa salama wanapofanya kazi yao ya kuchimba madini.

Pia amewashauri wachimba madini kuhakikisha kwamba wanapokuwa katika maduara ya uchimbaji madini wahakikishe kwamba wale wachimbaji wanaoingia pale ni wale wenye ufahamu na shughuli nzima ya uchimaji wa madini kwa siyo kila mtu anaingia kwa sababu tu ni shughuli ya kuwapatoa kipato.

Aidha amewashauri wawekezaji kufika Jeshi la Zimamoto pindi wanapotaka kufanya uwekezaji wao kwa ajii ya ushauri na kupewa na maelekezo yanayohusiana na uchimbajiwa madini.

Mbali na shughuli za uchimbaji wa madini mkoa wa Lindi una fursa nyingi katika shughuli za uwekezaji hasa uwekezaji wa gesi asilia.

“Katika eneo hili kuna viashiria vingi vya moto, ila jeshi letu limejipanga kutoa elimu kwa jamii ambayo itakuwa karibu na maeneo ya uchumbaji wa gesi jinsi ya kuishi salama katia maeneo hayo na namna ya kukabiliana na majanga ya moto yanayoweza kutokea,” amesema Mapunda na kuongeza kuwa

“Moja ya eneo ambalo tualielekeza sana kwa jamii ni kwamba waepuke uchomaji wa moto hovyo katika maeneo yao,kama tunavyojua watu wengi wa mikoa ya Lindi na Mtwara wengi ni wakulima wa mazao ya kibiashara kama korosho ufuta na mazao mengine,

“Sasa kumekuwa na desturi ya kuandaa mashamba kwa kuchoma moto ,lakini pia kumekuwa na desturi ya watu wengi kukata misitu na kuchimba bila kujua ni wapi na kumepita nini,” amesema Mapunda.

Kuifuatia hali hiyo amewashauri wananchi waishio mikoa ya Lindi na Mtwara kuwa makini na zile zinapitisha gesi na kwamba wajue njia zinazopitisha gesi na kujua jinsi gani wanaweza kuishi bila kuleta athari wala uharibifu wowote utakaopelekea uvujaji wa gesi.

Amewaasa wananchi kutembelea viwanja vya maonyesho hasa katika banda la Zimamoto na Ukoaji ili waweze kupata elimu inayohusiana na masula ya moto na uokoaji.

Hata hivyo, mkazi wa mjini Ruangwa, Swaumu Hassan ameiomba Serikali kuwatupia jicho Zimamoto na Uokoaji kwenye suala la magari na watumishi kwani ni wachache.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...