Na Mwandishi wetu Dodoma

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania

(JWTZ) limetoa ufafanuzi kwa Jamii ya Watanzania kuhusiana na kadhia inayokinzana na katazo la kisheria la raia kuvaa, kumilikie au kuuza mavazie ya kijeshi bay yanayopelekea kufanana na sare za kijeshi.

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linakataza kuvaa mavazi ya jeshi ambayo ni pamoja na kombati (vazi la mabaka mabaka), makoti, tisheti, suruali, magauni, kofia, viatu, mabegi na kaptula zenye rangi zinazofanana au kushonwa katika mitindo ya kijeshi.

Kaimu Mkurugenzi wa habari na uhusiano Makao Makuu ya Jeshi (JWTZ) Luteni Kanali Gaudentius Ilonda ametoa kauli hiyo Leo Jijini Dodoma mbele ya wanahabari, ambapo amesema katazo hilo la mavazi ni kwa mujibu wa kifungu cha 99 cha sheria ya Ulinzi wa Taifa (NDA) Sura ya 192 sheria namba 24 ya mwaka 1966 iliyofanyika marejeo mwaka 2002.

"Zipo Taasisi zinazowashonea watumishi wake sare za aina hiyo, wapo pia wafanyabiashara wanaoingiza nchiniw mavazi ya Aina hiyo na kuyauza kwa baadhi ya raia kupitia katika maduka au maeneo Yao ya biashara."

Luteni Kanali Ilonda amesema wapo baadhi ya watu ambao kwa kuyatumia mavazi hayo wamekuwa wakiwatapeli wananchi na wengine kufanyae vitendo viovu ambao piae wamekuwa wakidhaniwa kuwa nie Wanajeshi, vitendo hivyo ni vya uvunjifu wa sheriae za nchi na havipaswi kufumbiwa macho na halie hiyo ikiachwa inaweza kuhatarisha ulinzi na usalama WA nchi.

Aidha Luteni Kanali Ilonda amesema Jeshi la Wananchi Tanzania linawasihi na kuwaomba Wananchi kusalimisha mavazi hayo ndani ya siku Saba (7) na baada ya siku hizo Saba atakayekutaa na mavazi hayo atachukuliwa hatua za kisheria

Hata hivyo Jeshi hilo linawafahamisha wananchi kuwa utekelezaji wa majukumu yake ya msingi na mengineyo unategemea Sana ushirikiano mzurie wa wananchi wote.

"Mahusiano ya Jeshi letu na wananchi ndiyo mhimili mkubwa ndani ya nchi na nje ya nchi, sio hekimae kwetu kulumbana kwa namnae yoyotee Ile na baadhie ya wananchi wenyee mavazie yaliyokatazwa ndiyo maana tunatoa siku sabae kuyasalimisha bila kuchukuliwa hatuae ili kuepukae usumbufu kwa ambayee hatayawasilisha atakuwa na nia ovu na dhamira mbaya.


Kaimu Mkurugenzi wa habari na uhusiano Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Luteni Kanali Gaudentius Ilonda wakati akizungumza na wanahabari Leo Jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...