Na.Khadija Seif ,Michuziblog 

KATIKa kuunga mkono juhudi za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan za kutangaza na kukuza utalii wa Tanzania, kampuni ya HB Sacs Boxing inatarajia kuandaa pambano la 'Royal Tour Boxing Kanda ya Ziwa litakalofanyika Septemba 30 mwaka huu jijini Mwanza katika Ukumbi wa Rock City Mall.

Akizungumza na Wanahabari Promota wa pambano hilo, Hassan Kumbucha amesema lengo la kuandaa mtanange huo ni kutangaza utalii, kuhamasisha mchezo huo Kanda ya Ziwa na kuleta uzalendo.

"Kampuni yetu imekuja kitofauti sana tunahitaji kutoa fursa za utalii, pia kuleta hamasa Kwa mabondia wa kanda ya Ziwa na kuunga mkono Rais Dk. Samia, "alisema Kambucha.

Promota huyo ameweka wazi kuwa  pambano kuu litakuwa kati ya bondia mtanzania, Fadhili Majiha 'Stopper' dhidi ya Renz Rosia raia wa Ufilipino kuwania mkanda wa Ubingwa wa ABU.

"Kabla ya pambano la Majiha na mfilipino kutakuwa na mapambano ya vijana ambayo yatafanyika Karagwe Buringi Septemba 25 mwaka huu baada hapo wataenda kuangalia utalii Chato Septemba 26.

Bondia, Fadhili Majiha amesema amefurahi kupata nafasi hiyo ya kucheza katika pambano kubwa ambalo linatangaza utalii wa ndani.

Ambapo mara nyingi amekuwa akikosa nafasi ya kucheza, ila kupitia kampuni hiyo atapambana na kuonyesha uwezo wake.

"Pongezi kwa kampuni ya HB Sacs Boxing Kwa kuandaa pambano hili na kuniamini, nimejiandaa vema na bado naendelea na mazoezi chini ya kocha wangu, Kwa me Hamisi watanzania waniombee dua mkanda ubaki nyumbani."

Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC), Nassoro Chuma ameeleza kuwa  jambo nzuri ni kuona wadau wa michezo wanamuunga mkono Rais Dk. Samia.

Aidha mabondia ambao watapanda ulingoni siku hiyo wanatakiwa kutoa burudani na kucheza Kwa viwango vikubwa.

Pamoja na Majiha na Mfilipino mapambano mengine ambayo yatasindikiza pambano hilo ni Saleh Kassim dhidi ya Freddy Sayuni wakati Stumai Muki atacheza na Engine Kayange huku Shomari Milundi na Abdullah Rashid na Ahmed Pelembela ataonyesha ubabe na Issa Maneva.

Wengine Luckman Ramadhani atapigana na Khalid Karama wakati John Chua dhidi ya Ramadhani Kumbele huku Said Mkola akiwa na kibarua kizito na Francis Miyeyusho.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...