WIZARA ya Mifugo na Uvuvi kupitia kituo cha Taifa cha Uhimilishaji(NAIC) imefanikiwa kusambaza mbegu bora za mifugo zaidi ya 150,000 kwa wafugaji kote nchini katika mwaka wa fedha 2022/2023.
Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkuu wa Kituo hicho Agosti 6,2023, Dk.Dafray Bura katika maonesho ya Kilimo Mifugo na Uvuvi NanenaneKanda ya Kaskazini yanaoendelea mkoani Arusha
Amesema mbegu hizo zinazozalishwa na kituo hicho zimeonesha kuleta tija kwa wafugaji baada ya kutoa matokeo chanya kwa mifugo hiyo kuwa na uwezo wa kutoa maziwa mengi kuanzia lita 35 hadi 40 kwa ng’ombe mmoja.
“Mbegu zetu zimeonesha matokea mazuri mfano leo tumefanya paredi ya ng’ombe wa maziwa kuna ng’ombe alikua anatoa lita 38 hadi 40 kwa mkamuo ambao ni moja ya matokea yaliyotokana na madume yetu ambayo mbegu zao tumesambaza kwa wafugaji, ” amesema
Amebainisha kwasasa kituo kina aina tisa za madume ya mbegu ambapo licha ya kuzalisha mbegu hizo kwa ajili ya wafugaji pia kituo hicho kinatoa mafunzo kwa watu wanaotaka kufanya kazi ya uhimilishaji
Amebainisha lengo la Serikali ni kuwafanya wafugaji nchini kuacha ufugaji wa kuhamahama na kuingia kwenye ufugaji wa kisasa ambao unatumia mifugo michache inayotokana na mbegu bora na kupata mazao mengi ambayo yatawainua kiuchumi tofauti na ilivyo sasa
“Tunazo aina tisa za mbegu kwa sasa ambapo kwa ngombe wa maziwa tuna aina ya Frishan, Ashaya na Jezze, nyama na maziwa tuna ng’ombe aina ya Flegvi, Simento na Saiwan na nyama tu.
"Tuna aina ya Borani na Bonsmara na kazi yetu kubwa ni kuzalisha hizi mbegu na kuzisambaza kupitia wahimilishaji kulingana na mhitaji nchini, ” amesema
Amefafanua katika kuhakikisha elimu ya ufugaji kwa kutumia mbegu bora zinawafikia wafugaji wengi kituo hicho kinaendelea kutoa elimu katika kanda zote yanapofanyika maonesho ya Nanenane, hivyo wafugaji wanapaswa kutumia fursa hiyo ili weweze kufuga kisasa
Kwa upande wake mmoja wa wanufaika wa mbegu bora ya uhimirishaji Emmanuel Nanyaro ambaye ni mfugaji kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Arumeru Arusha amesema kwa sasa anapata faida kubwa baada ya kupata ng’ombe mwenye uwezo wa kutoa maziwa hadi lita 40
Amesema baada ya kupata faida hiyo sasa ameamua kujitolea kutoa elimu kwa wafugaji wengine ili kusaidia wafugaji kutambua umuhimu wa kutumia mbegu bora zinazopatikana katika kituo cha uhimilishaji NAIC ili waweze kujiinua kiuchumi.
“Nawashauri watu wanaotaka kuingia kwenye ufugaji waje tupeane elimu ili waweze kuwa na ng’ombe bora maana ukitaka kufuga lazima uwe na ng’ombe bora ambao utapata mbegu kutoka kituo cha NAIC kilichopo hapa Arusha, ” amesema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...