Na  Mwamvua Mwinyi,Kibaha

Mbunge wa jimbo la Kibaha Mjini,Silvestry Koka amehimiza Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Kibaha Mjini, kubuni miradi ambayo itaona inafaa ili kujiimarisha kiuchumi ambapo yuko tayari kuhakikisha inatekelezeka kwa gharama yoyote.

Aidha ameihakikishia Jumuiya hiyo ushirikiano katika kutekeleza majukumu ya Jumuiya na kukijenga Chama. 

Koka alieleza, hayo wakati wa kufunga semina ya mafunzo kwa wajumbe wa Baraza la Wazazi Wilaya yaliyofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya Mji Kibaha.

Hata hivyo ,aliwapongeza viongozi wa Jumuiya ya Wazazi kwa namna wanavyo wajibika kwa nyakati tofauti katika ujenzi wa chama.

Kwa kuthibitisha ushirikiano huo Koka alisema tayari ipo fedha kwajili ya hatua za awali kuelekea kutekeleza miradi mbalimbali ambayo Jumuiya ya wazazi imebuni na ile ambayo wataendelea kuibua kwa masilahi mapana ya Jumuiya hiyo.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...