Halmashauri ya Wilaya ya Magu itaendelea kutoa elimu kwa wakulima , wafugaji na wavuvi kuhusu mbinu bora za kilimo na ufugaji wa kisasa ili kuongeza tija katika shughuli za uzalishaji kwenye  wilaya hiyo  na kuinua kipato cha wakulima.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Kilimo , Mifugo na Uvuvi Halmashauri ya Wilaya ya Magu Ndugu Mohamed Ramadhan Kyande wakati wa maonesho ya nanenane 2023 yenye kauli mbiu"VIJANA NA WANAWAKE NI MSINGI IMARA WA MIFUMO ENDELEVU YA CHAKULA" yanayofanyika katika viwanja vya Nyamhongolo Jijini Mwanza ambapo alibainisha kuwa Magu imejipanga kuendelea kufanya vizuri katika maonesho ya Nanenane mwaka huu.

Ameongeza kuwa katika maonesho ya mwaka huu banda la Halmashauri ya Magu limejipanga kuonesha bidhaa za kilimo, mifugo na uvuvi kulingana na kauli mbiu ya Nanenae mwaka huu ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuwa na mifumo endelevu ya chakula.

Amesema katika maonesho hayo banda la Halmashauri ya Wilaya Magu limegawanyika katika sehemu tatu ambazo alizitaja kuwa ni sehemu ya Uzalishaji, sehemu ya uchakataji na sehemu ya masoko.

Ameongeza kuwa katika sehemu zote wapo wataalamu wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi  kwa minaajili ya utoaji elimu kuhusiana na ukulima na Ufagaji bora wa wanyama na samaki.

Bwa. Kyande alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wananchi kutembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Magu katika maonesho ya Nanenane 2023  kwaajili ya kujionea na kujifunza mambo mbalimbali ya kilimo, uvuvi na ufugaji wa kisasa unaoendana na mabadiliko ya Sayansi na teknolojia.Afisa Kilimo Halmashauri ya Wilaya ya Magu akielezea Teknolojia ya ufugaji wa samaki kisasa kwa wananchi waliotembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Magu katika Monesho ya Nanenane 2023 yanayofanyika katika viwanja vya Nyamhongolo Jijini Mwanza.

Mtaalamu wa Teknolojia ya  mkaa mbadala KUNI SMART, Bi.  Witness Kashuji akitoa maelezo ya teknolojia hiyo inavyoweza kutunza mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi kwa kutumia kuni mbadala katika Monesho ya Nanenane 2023 yanayofanyika katika viwanja vya Nyamhongolo Jijini Mwanza.
Afisa kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu Ndg. Valerian Mwanga akimpa maelezo kuhusu Mbegu za zao la mahindi  Mkuu wa idara ya kilimo, mifugo na uvuvi wa Halmashauri ya Magu Ndg. Mohamed Ramadhan Kyande wakati akimpitisha sehemu mbalimbali za banda la Magu kwenye maonesho ya Nanenane mwaka 2023 yanayofanyika katika viwanja vya Nyamhongolo Jijini Mwanza.

Baadhi ya vipando vilivyopo kwenye  sehemu ya uzalishaji katika banda la Halmashauri ya Wilaya ya Magu viwanja vya Nanenane Nyamhongolo Jijini Mwanza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...