Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amefurahishwa na jitihada zilizofanywa na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) za kuandaa Mkakati wa Taifa wa Kubidhaisha Kiswahili Ndani na Nje ya Nchi kwa miaka kumi (10) kuanzia 2022 hadi 2032.
Mkakati huo ulioanza utekelezaji wake mwaka 2022 umelenga kuhakikisha lugha ya Kiswahili inakuwa bidhaa itakayosaidia kutatua changamoto ya ajira kwa wasomi wa Kiswahili walio ndani ya nchi.
Mhe. Chana ameagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha zinashiriki katika utekelezaji wa mkakati huo, kwani ni mkakati wa taifa na kila Mtanzania anapaswa kushiriki katika kuutekeleza. Katika hatua nyingine, Mhe. Pindi Chana ameliagiza BAKITA kuhakikisha kila halmashauri nchini inapata nakalamango na nakalatepe ya Mkakati wa Taifa wa Kubidhaisha Kiswahili.
Mhe. Waziri Pindi Chana amesisitiza kuwa mkakati huo unatekelezwa kwa asilimia mia moja kwa sababu utakuwa chachu ya ongezeko la pato la taifa kwa kuwa lugha ya Kiswahili inatuimika kuvuta watalii nchini. Waziri ameongeza kuwa kwa sasa soko la ukalimani limezidi kukua na kwa sasa Jumuia ya Afrika Mashariki inahitaji na Umoja wa Afrika wanahitaji wakalimani.
Akiwasilisha Mkakati huo, Katibu Mtendaji wa BAKITA, Bi. Consolata Mushi, amesema kuwa dira ya Mkakati wa Taifa wa Ubidhaishaji wa Kiswahili ni kuwa na mfumo madhubuti wa kitaasisi katika kuratibu, kusimamia na kukuza maendeleo ya Kiswahili kitaifa, kikanda na kimataifa na dhima ya mkakati huo ni Kusimamia, kuratibu na kushiriki kikamilifu katika kustawisha maendeleo na matumizi ya Kiswahili kitaifa na kimataifa.
Bi. Consolata ameeleza kuwa, mkakati huo umebainisha fursa mbalimbali za lugha ya Kiswahili ikiwamo kuuza machapisho mbalimbali ya Kiswahili ili kuinua vipaji na hali ya waandishi wazawa. Bi. Mushi amesema kuwa lengo kuu la mkakati ni kukuza Kiswahili ili kiwe chachu ya maendeleo ya taifa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...