Na. Dennis Gondwe, DODOMA

AMANI na usalama wa Kata ya Chang’ombe inatokana na jinsi jamii inavyowalea watoto katika misingi bora na maadili mema.

Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu Afisa Mtendaji wa Kata ya Chang’ombe, Daria Kapinga alipokuwa akiongea na wananchi wa Mtaa Mazengo kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Chama Cha Mapinduzi na kufanyika katika Ofisi ya CCM Tawi la Chang’ombe Magharibi.

Kapinga alisema “ninatamani kuzungumza na mitaa miwili Mazengo pamoja na Msamalia suala la amani na ulinzi. Mitaa yetu imekuwa ni mitaa ambayo inatajwa sana kwenye sifa mbalimbali. Lakini chanzo nilichobaini ni kutoka kwenye mizizi ambapo ni kwa watoto wetu, kwenye malezi ya watoto wetu tumeshindwa kuidumisha amani, tumeshindwa kudumisha ulinzi kwa sababu ya malenzi tuliyonayo kwa watoto wetu. Malezi yasiyo mema kwa watoto matokeo yake ya muda mrefu yanapelekea kwenye uvunjifu wa amani na usalama”

Kapinga alisema kuwa imefika hatua mzazi analalamika kuwa mtoto wake ameshindikana na kusema hiyo ni hatua mbaya kimaadili.

 “Hakuna mzazi anayetamani hata siku moja mtoto wake aharibikiwe, ila siku hizi hayo mambo yamekuwa ni ya kawaida katika jamii zetu, imefikia hatua mzazi anakwambia mtoto amemshindwa. Hakuna mtoto ambae atalelewa na ulimwengu, kwenye suala la malezi usisubiri mtoto afike kwenye umri fulani anza nae sasa akiwa mdogo. Hatutakuwa na Chang’ombe iliyo bora kama tusipokubali kubadilika na kuwalea watoto wetu. Leo hii wengi wanalalamika wanafanyiwa vitendo vya kikatili lakini tunaowaogopa ni watoto tuliowazaa wenyewe. Niwaombe sana tubadilike katika kuwalea watoto wetu. Wazazi wetu wasingetulea vizuri hata hawa viongozi wasingekuwepo” alisema kapinga.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...