Njombe

Mbunge wa Jimbo la Makambako mkoani Njombe Deo Sanga (Jah people) amekosoa wanaopotosha kuhusu uwekezaji na mkataba wa bandari ya Dar es Salaam na kudai kuwa wao wabunge ndio waliokubali kuwa na muwekezaji katika bandari kwa kuwa hakuna ambaye angeacha uwekezaji wa Tilioni 26.

Sanga ameeleza hayo kwenye kikao cha baraza la madiwani robo ya nne na kufunga mwaka 2022-2023 cha halmashauri hiyo ambapo amesema DP World watakapowekeza fedha nyingi zitapatikana na kwenda kujenga miradi mingine.

"Sisi ndio wabunge tuliokubali kuwa namwekezaji ndani ya nchi yetu katika bandari ya Dar es Salaam,hawa (DP World) ambao ni wawekezaji wapya watalipa Tilioni 26 ambayo ina tija na ni zaidi ya  robo tatu ya bajeti yetu sasa watu wengine wanapotosha"amesema Deo Sanga

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...