Na Mwandishi wetu, Simanjiro
DIWANI
wa Kata ya Edonyongijape Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Jacob
Kimeso amechaguliwa kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri
hiyo kupitia CCM.
Katika
uchaguzi huo uliokuwa na wagombea saba, Kimeso ambaye ni Makamu
Mwenyekiti aliyemaliza muda wake wa mwaka mmoja ameshinda kuwa mgombea
kwa kupata kura 16.
Kimeso
akizungumza baada ya kuchaguliwa kugombea nafasi hiyo ya mwaka mmoja,
amewashukuru madiwani hao kwa kuwa na imani naye hadi kumrudishia tena
umakamu mwenyekiti.
Amesema
imani huzaa imani, amewaahidi kuendelea kutumikia nafasi hiyo ya
kumsaidia Mwenyekiti, kwa lengo la kufanikisha maendeleo ya wilaya ya
Simanjiro yenye neema tele.
"Ndugu
zangu wahehimiwa madiwani nachukua nafasi hii kuwashukuru kwa
kunichagua tena kwa mara ya pili kwa nafasi ya makamu mwenyekiti wa
halmashauri nawaahidi sitawangusha tuko pamoja kazi iendelee," amesema
Kimeso.
Mkuu wa Mkoa wa
Manyara, Queen Sendiga ambaye ndiye amesimamia uchaguzi huo amewataka
madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro kuachana na makundi ya
kisiasa, wajikite kupambania maendeleo ya watu waliowachgua.
Sendiga
amesema madiwani wote wa Simanjiro wanatokea CCM, hivyo wahakikishe
wanaondokana na makundi ya uchaguzi na kujikita kwenye suala la
maendeleo.
"Uchaguzi tuu
wa kumpata mgombea wa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri kupitia CCM
umechukua siku nyingi kufanyika, sababu ya malumbano, sasa leo
umefanyika acheni migogoro fanyeni kazi," amesema Sendiga.
Amesema
anatarajia baada ya uchaguzi huo kumalizika Simanjiro, kitakachofuata
ni umoja na maendeleo na siyo kuendeleza malumbano na migogoro isiyo na
tija.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...