Na Muhidin Amri,Tunduru

MKUU wa wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro,ametoa wito kwa viongozi wa Dini,viongozi wa kimila na na wazee kusaidia suala la malezi kwa watoto na vijana kimaadili ili kuweka mustakabali wa Taifa na watu wake kwenye mikono salama.

Amewataka wazazi wilayani humo, kutenga muda kuzungumza na watoto wao kama njia ya kuwajenga kiimani ambayo itasaidia sana kufuata mafundisho ya Dini zao na makatazo MwenyeziMungu ili kuzuia uwezekano wa kushiriki kwenye vitendo vya ukiukaji wa maadili vinavyoendelea kufanywa na baadhi ya watu hapa nchini.

Mtatiro amesema hayo jana,alipokuwa akizungumza na waumini wa Dini ya Kiislam katika Ibada maalum ya Ijitimai iliyofanyika katika msikiti Mkuu wa wilaya ya Tunduru.

Alisema,vijana wakifundishwa vizuri mila,desturi na kushika mafundisho ya dini na wakawa na hofu ya Mwenyezi Mungu maovu mengi ikiwemo ndoa za jinsia moja,ulawiti na unyanyasaji wa kijinsia vitapungua kwa kiwango kikubwa hapa nchini.

Alisema kuwa,serikali inaambua umuhimu wa madhehebu ya Dini na itaendelea kushirikianakatika kujenga maadili mema kuanzia ngazi ya familia na jamii kwa ujumla.

Aidha,amewaomba waumini wa Kiislam na madhehebu mengine ya Dini wilayani humo kuliombea Taifa na Rais wake Dkt Samia Suluhu Hassan ili aweze kutekeleza vema mipango ya maendeleo.


Mkuu wa wilaya ametumia nafasi hiyo kukemea vikali vitendo vya ukatili na unyanyasaji dhidi ya watoto wa kike na kiume na kuhaidi kwamba serikali ya itahakikisha inaongeza nguvu katika kupambana na ukatili na kuimarisha ulinzi kwa watoto hao.

Amewakumbusha viongozi wa dini na waumini wao,kuendelea kukemea vitendo na maneno kutoka kwa baadhi ya watu wakiwemo wana saiasa yanayoweza kuwagawa Watanzania na kusisitiza kuwa,sisi sote ni wamoja.

Pia Mtatiro, amewasa wazazi na walezi na walezi kuweka mifumo imara ya ulinzi kwa watoto kuanzia ngazi ya familia,mtaa,mashuleni na sehemu nyingine ili kulinda haki na ustawi wa watoto na kuwaepusha na vitendo vya ukatili vinavyofanywa na watu wazima katika jamii.

Kwa upande wake mwakilishi wa Mufti Mkuu wa Tanzania Shekhe Arifa Surya alisema,siku tatu za Ibada hiyo iliyoambatana na Dua ya kuliombea Taifa,wamefika kwenye vijiji mbalimbali kwa lengo la kuwakumbusha Waislam na wasio waislam kudumisha amani kuishi katika maadili mema.

Shekhe Surya ambaye ni Mkurugenzi wa Da’awa na Tabligh kutoka Baraza kuu la Waislamu Tanzania(Bakwata) alisema, hivi sasa kumekuwa na mmomonyoko mkubwa wa maadili.

Alisema,baadhi ya watu kutoka mataifa ya nje wanafanya jitihada kubwa zinazokwenda kinyume na utu wa Binadamu na mafundisho ya MwenyeziMungu kwa kuwafundisha watoto wa kiume kujiingiza kwenye ndoa za jinsia moja.

Aidha alisema,Ibada hiyo ililenga kuwakumbusha wanaume kuhusu kusimamia vyema nyumba zao ili kupata kizazi kilicho bora badala ya kumwachie jukumu hilo mwanamke kwani katika malezi ya watoto mwanamke akikaa sawa Taifa letu litakuwa na jamii ya watu wema.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri kuu ya Bakwata wilayani Tunduru Abdala Kawanga,ameishukuru serikali kwa kuendelea kushirikiana na viongozi wa Dini hali iliyowezesha wilaya hiyo kuwa na utulivu na wananchi kupata muda wa kufanya shughuli zao za uzalishaji mali.

Amempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan,kupeleka mbolea za bure kwa wakulima wa zao maarufu la korosho.

Mkuu wa wilaya yaTunduru Julius Mtatiro akitoa salamu za serikali kwa waumini wa Dini ya Kiislam baada ya kukamilika kwa Ibada ya Ijitimai iliyofanyika katika msikiti mkuu wa wilaya mjini Tunduru,katikati ni mkurugenzi wa Da'awa na Tabligh kutoka Baraza kuu la Waislam Tanzania Bakwata.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...