Na Mwandishi wetu, Simanjiro
WAKAZI wa Tafara ya Terrat Wilayani Simanjiro Mkoani Ma. Wakazi wa Tarafa ya Terrat, Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wameiomba Serikali kuwapatia askari wa kike kwenye kituo cha polisi Komolo, kwani wanawake wanakamatwa na askari wa kiume.
Hayo yameelezwa kwenye kongamano la mradi wa Tanzanite uchumi imara wa mwanamke mji mdogo wa Mirerani lililoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Civil Social Protection Foundation (CSP).
Mmoja wa wakazi wa kata ya Terrat, Scola Lukumay amemuomba mkuu wa wilaya ya Simanjiro Dk Suleiman Serera kuwasaidia ili waweze kupata askari wa kike.
“Kwenye kituo hicho cha polisi Komolo hakuna askari polisi wa kike hivyo wanawake wanakamatwa na askari wa kiume hivyo kukiuka haki za binadamu tunaomba askari wa kike,” amesema.
Amesema ingelikuwa vyema serikali kuangalia jambo hilo kwa jicho la tatu ili kuwepo na usawa wa kijinsia wa askari wa kike, kwani kwa sasa wananchi wa eneo la tarafa hiyo wanakwazika.
Hata hivyo, mkuu wa wilaya ya Simanjiro Dk Suleiman Serera amesema amepokea ombi hilo na atahakikisha jitihada za dhati zinafanyika ili askari wa kike apatikane katika kituo hicho.
“Hilo nimelichukua nitazungumza na OCD (mkuu wa polisi wa wilaya) ambaye bado ni mgeni ili aweze kupanga askari wa kike kwenye kituo hicho cha polisi Komolo,” amesema Dk Serera.
Mwanasheria wa CSP, Eliakim Paulo amesema lengo la kongamano hilo ni kuangalia changamoto na kero zinazowapata wanawake wanaozunguka machimbo ya mdini ya Tanzanite.
“Tumeona tufuatilie ahadi zilizotolewa hivi karibuni tulipokutana na baadhi ya viongozi wa serikali kama zimetimizwa katika sekta mbalimbali,” amesema Paulo.
Kongamano hilo limebaini kuwa asilimia kubwa ya changamoto zilizokuwa zinalalamikiwa na wanawake wa eneo hilo zimefanyiwa kazi hivyo kuwapongeza CSP walioandaa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...