Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mhe.Dkt, Samia Suluhu Hassan akimshukuru Mkurugenzi mtendaji wa Camel Oil, Edha Abdallah kushoto kwake, baada ya uzinduzi wa mradi wa kituo cha michezo cha kufurahisha watoto kuanzia miaka mitano hadi 18, unaofadhiliwa na kampuni ya Camel Oil Tanzania ambapo utagharimu zaidi ya bilioni 1 na itachukua hadi miezi 12 kukamilika.
Rais Samia alimsifu mkurugenzi huyo kwa kuwa mtekelezaji kwa vitendo. Utakapokamilika unatarajiwa kuwanufaisha wakazi wa Kibuteni, Kizimkazi, Kusini Unguja. Mbali ya michezo, pia kutakuwa na kumbi za sherehe na sehemu za kupumzikia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...