Na Said Mwishehe, Michuzi TV

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amesimamisha kuanza kwa soko jipya la Mbagala Zakhiem kwa muda wa siku saba ili afanye uchunguzi kubaini waliotoa fedha kwa madalai ili wapatiwe maeneo ya kufanya biashara ndani ya soko hilo.

Chalamila ametoa kauli hiyo mbele ya viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Temeke na wananchi baada ya kuzindua soko hilo jipya ambalo ujenzi wake umegharimu sh.bilioni 2.2 ambazo zimetolewa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ambapo ameeleza pamoja na kulizindua na kutakiwa kuanza kufanya kazi leo, amesitisha kwa muda uzindizi huo kwa ajili ya kufanya uchunguzi.

“Kama umeliwa fedha yako kwa kuambiwa utapata eneo kwenye soko hili ukitoka hapa kamwabie uliyempa Chalamila kasema nirudishie hela yangu kwasababu hapo sitapata.Mimi moja ni moja na mbili ni mbili sitakuficha, na madalali wa aina hiyo wapo , wapo ambao si watumishi wa umma na wapo watumishi wa umma

“Nimesema kwenye utawala ambao mimi nipo hapa ni Mkuu wa Mkoa kwa leo ni lazima watu tuwe na nidhamu na adabu ya kufuata misingi ili mambo yaende vizuri.

“Asitokee hata mmoja kujiona yeye ni dalali mzuri , mimi nitakunyoosha vizuri hata kama ni dalali wa miaka mingi.Tunahitaji watu waelewe kwamba kama hili soko linakwenda kwa utaratibu gani.

“Leo hii walioomba wako zaidi ya 2000 lakini maduka haya yako 150 tu , na madalali wengine watu wa hovyo wanapita kwenye migongo ya wanaosema walikuwapo,”amesema.

Amesisitiza amesimamisha kwanza kazi kwa soko hilo ambalo tayari amelizindua ili kieleweke vizuri huku akitoa namba yake ya simu kwa ajili ya wote ambao wametoa fedha kwa madalali ili kwa kigezo watapa maeneo ya biashara watoe ushahidi ili yeye nitachomoka na huyo mtu le oleo

“Awe Diwani, awe nani, awe Mwenyekiti, awe ni dalali nitapita naye kwenye mkanda mmoja namna hii kwasababu Rais wetu Dk.Samia Suluhu Hassan ametoa Sh.bilioni 2.2 kwa ajili ya ujenzi wa soko la Zakhem.

“Zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa soko hilo na hakuna mtu aliyechangishwa kujenga soko hilo.Na nitakapokamilisha uchunguzi huo tutangalia saa na bei ya pango ambayo itakwenda kulingana na thamani ya ujenzi wa soko.

“Hili soko linahitaji kuboreshwa na kufanyiwa matengeneza ya miundombinu itakapoharibika,ukifanya zile bei za msaada  juu wanakuja madalali ambao wao ndio wanakusanya kile kidogo kinakwenda serikalini hiyo nimekataa,”amesema.

Ameongeza Halmashauri ya wilaya ya Temeke ipange bei ya pango na wampe taarifa na wakimdanganya atakwenda kuuliza mwenyewe kwa wafanyabiashara.

Aidha ametoa utaratibu wa kugawa mabanda ya biashara katika soko hilo ambapo amependekeza ugawaji uzingatie makundi yote kwa maana ya watu wenye mahitaji maalum kama walemavu, wanawake na wanaume.

“Mnaweza kugawa kwa mfano kibanda namba moja mpaka 20 watakaopewa kwa bei hiyo hiyo watu wenye ulemavu,labda 20 mpaka 50 kwa bei hiyo hiyo wanawake tu, 70 mpaka 100 wanaume ili makundi yote yawe sehemu ya soko hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila( katikati) akiwa na viongozi wengine wa Halmashauri ya Wilaya ya Temeke baada ya kukata utepe kuashiria kuzindua soko jipya la Zakhiem ambalo ujenzi wake umegharimu Sh.bilioni 2.2
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila akizungumza na wananchi kuhusu masuala mbalimbali yakiwemo ya mipango ya Serikali katika kuendelea kuiboresha Dar es Salaam
Mkuu wa Wilaya ya Temeke mkoani  Dar es Salaam Mobhare Matinyi akieleza jambo  kabla ya kuumkaribisha Mkuu wa Mkoa kuzungumza na wananchi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...