Pichani ni kiongozi mkuu au Shibu-cho  wa Chama cha Jundokan Karate-Do Tanzania Sensei Rumadha Fundi (Go Dan - 5th Dan)  akiwa na washiriki wengine160 toka nchi zaidi ya 18 katika mabara manne kama vile; Ulaya, Marekanikaskazini (Alaska) na kusini (Argentina), Japan (Okinawa), Afrika (Angola naTanzania), na mashariki ya kati (Israel).

Sensei Rumadha na wenzake walikusanyika katika kisiwa cha Sicily huko nchini Italia kwa siku tatu toka Julai 27, 2023 kwa mafunzo maalum ya chama hicho yanayofanyika kila mwaka ndani ya bara la Ulaya na kuwashirikisha wanachama wenza toka mabara tofauti ikiwemo nchi za Afrika kama Tanzania na Angola.
Kongamano hilo huwa na lengo la kuwanoa wakufunzi wa ngazi zote za mikanda ya karate hususani walimu wakuu. Jopo la walimu “Masters” toka Naha,Okinawa, Japan visiwa vya chimbuko la karate, huteuwa walimu hao na kuendesha
semina hizo.
“Semina hizi za kimataifa hufanywa na mitindo yote ya karate duniani, lakini sasatunaongelea chama cha Jundokan karate hapa”, alisisitiza sensei Rumadha. Mpakasasa hivi nimeshiriki semina (Gasshuku) nyingi sana na kwa miaka mingi tokeamwaka 1991 chini ya masters wakubwa toka Okinawa, Japan kama vile MorioHigaonna, Teruo Chinen, Matasaka Muramatsu, Tetsu Gima,Tsuneo Kinjo na
Kancho Yoshihiro Miyazato.
“Sidhani kama kuna sensei yeyote hapa Tanzania aliyewahi shiriki semina nyingi na masters wa ngazi juu kabisa duniani kulingana nami kiukweli”, alisemasensei Rumadha mwenye uzoefu wa karate wa zaidi ya miaka 45 sasa naanashikilia ngazi ya dan 5 aliyopewa na master Yoshihiro Miyazato zaidi ya miaka
mitano iliyopita baada ya kufuzu mtihani toka chama cha Jundokan Karate-do
Goju Ryu.
Tanzania, pia imepata mwaliko mwingine kusheherekea miaka 70 ya chama chaJundokan kianzishwe na mwasisis wake master Eiichi Miyazato 1957 huko Naha,Okinawa ,Japan, maadhimisho hayo yatafanyika mwezi Novemba, 2024.
Mandeleo ya karate nchini hutegemea sana jinsi gani kila chama kinavyoendeshwana wakuu wake. Hivyo ipo misingi inayofuata kuhakikisha kila mtindo na vyamavinaendeleza vipaji vipya vitakavyoendeleza Sanaa hii hapa Tanzania.Tumepata fursa ya kujifunza mengi na kuzungumza maendeleo na mbinu tofauti za karate.
Pia kuweza kukutana na kujuana na walimu (Masensei) toka nchimbalimbali. “Karate-Do au kwa jina linguine mwenendo wa karate ni kushirikimakongamano kama haya nakuwashirikisha masters wa mitindo yeyotekuhakikisha mbinu hazifuji au kuwa nakutu kimafunzo. Kila sensei huitajimasahihisho toka kwa wenzie wa ngazi za juu kiushirikiano, hivyo ndivyo tunafanya hapa.





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...