Na Mwandishi Wetu, Geita
MAMBO yanaonekana kuwa magumu kwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), baada ya kuahirisha mkutano wake kutokana na kukosa watu katika Kijiji cha Ilolangula, wilayani Mbogwe mkoani Geita.
Mkutano wa Lissu ulipangwa kufanyika leo saa sita mchana katika Kijiji hicho kama sehemu ya mwendelezo wa ajenda ya mikutano yao inayofanyika Kanda ya Ziwa.
Lissu aliingia kijijini hapo na timu yake kwa ajili ya mkutano huo, hata hivyo aliamua kuahirisha kuendelea na mkutano huo kama njia ya kuepuka aibu anayokutana nayo kutoka katika mikutano yao inayoonekana kukosa mvuto.
Chadema wamezindua ziara za mikoani wakianzia na mikoa ya Kanda ya Ziwa, ambayo hata hivyo imekuwa ikikosa watu huku chanzo cha hali hiyo kikitafsiriwa kama wananchi kuchukizwa na mwenendo wa Lissu kutoa lugha ya kuudhi anapokuwa anatoa hotuba yake.
Mwishoni mwa wiki iliyopita Lissu alifika mbali baada ya kuamua kutumia muda mwingi kuwakashifu viongozi wa serikali, akiwemo Hayati Benjamin Mkapa kwa kumuita mwizi wakati wa utawala wake na kuzalisha chuki dhidi ya wananchi wastaraabu nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...