Na Mwandishi Wetu

SHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limenyakua tuzo ya Kampuni bora ya mwaka Afrika kwenye sekta ya madini 2023 katika tuzo za Africa Company of the Year Award (ACOYA).

Tuzo hiyo imetolewa katika hafla iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali huku mchakato wa kutafuta washindi umefanywa na Kampuni ijulikanayo kama Eastern Star Consulting Group Afrika iliyopo nchini Kenya.

Akipokea tuzo hiyo kwa niaba ya shirika, Mkurugezi Mtendaji Dk. Venance Mwasse aliyeambatana na Menejimenti ya STAMICO, amesema tuzo hiyo imedhihirisha juhudi za shirika hilo katika kuinua sekta ya madini nchini.

Amesema hatua ya STAMICO kuwa kampuni bora kwa mwaka 2023 imekuwa chachu kwa shirika hilo kuongeza kasi ya utendaji ili kuwanufaisha Watanzania.

“Zaidi ya nchi 15 kutoka bara la Afrika zilishiriki kwenye kuwania tuzo hizi na STAMICO iliweza kuibuka kidedea kama Kampuni Bora ya Madini Afrika,” alisema.

STAMICO imekuwa mfano wa kuigwa Afrika kiasi cha kuivutia Wizara ya Madini na Uchumi wa Bluu nchini Kenya ambayo hivi karibuni viongozi waandamizi wa wizara hiyo walikuja nchini kujifunza namna shirika hilo linavyoendeleza shughuli za mnyororo wa thamani wa uchimbaji madini.

Walijifunza namna STAMICO imefanikiwa katika kuendesha shughuli za madini zikiwemo utafiti, uchimbaji, uchakataji, na biashara ya madini

Akizungumza katika hafla ya utoaji tuzo hizo, Mkurugenzi wa Africa Company of The Year Awards (ACOYA), Deogratius Kilawe amesema tuzo hizo zinajulikana kama Africa Company of the year Awards (ACOYA), mwaka huu 2023 ndio mara ya kwanza tuzo hizo kutolewa hapa Tanzania.

Aidha, Kilawe alizipongeza na kuzishukuru kampuni zote zilizoshiriki na kushinda.Lengo la tuzo hizo ni kuongeza ufanisi kwa kampuni katika utoaji huduma kwa wateja wao na wafanyakazi ili kuongeza uwajibikaji kazini.

“Mwisho wa tuzo hizi ni mwanzo wa maandalizi wa tuzo zijazo tunachukua changamoto zilizojitokeza mwaka huu kuboresha tuzo zijazo,

Mbali na STAMICO kupata tuzo katika hafla hiyo kuna baadhi ya Kampuni nyingine ziliweza kupata tuzo kama vile kampuni ya Ndege ya Uganda (Uganda Airlines) ambayo iliibuka kama Kampuni ya bora barani Afrika (Best Airline of the Year), Kampuni ya Kenya Wee Centre ilibuka mshindi wa kwanza kwa utunzaji wa mazingira na Kampuni ya Sintel Security ya nchini Kenya iliibuka mshindi kwenye kipengele cha uchapishaji nyaraka mbalimbali (printing solutions).





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...