Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amezungumzia umuhimu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS kujenga mizani katika Barabara kuu zinazoingia na kutoka mjini Kigoma.

Amesema kasi ya ujenzi wa barabara za kisasa mkoani Kigoma ni vema ikaendana na ujenzi wa mizani za kudhibiti uzito ili kuzilinda barabara hizo.

" TANROADS hongereni kwa kusimamia kwa karibu miradi ya ujenzi wa barabara inayoendelea katika mkoa huu, ni muhimu sasa muanze kujenga mizani ili kukamilika kwa barabara hizi kuendane na kuzilinda dhidi ya magari yanayozidisha uzito ", amesema Prof. Mbarawa.

Barabara kuu za Nyakanazi-Kigoma na Kigoma-Tabora ziko kwenye hatua muhimu za kukamilika kwa kiwango cha lami na hivyo kuvutia biashara na kukua kwa huduma za uchukuzi hivyo uwepo wa mizani za kisasa utasaidia kuzilinda barabara hizo ili zidumu kwa muda mrefu.

Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa amekagua ujenzi wa barabara ya Nduta Junction-Kibondo Mjini hadi Kibondo Junction yenye urefu wa KM 25 na Malagarasi-Ilunde KM 51.1 zinazojegwa na mkandarasi STECOL Cooperation Limited na kumtaka mkandarasi huyo kuongeza idadi ya vifaa na wataalam ili kasi ya ujenzi wa barabara hizo uendane na mahitaji ya Serikali ya kuufungua mkoa wa Kigoma kwa lami mapema iwezekanavyo mwakani.

" Hakikisheni mnaongeza kasi katika ujenzi huu Serikali haitasita kuwaondoa ikiwa mtashindwa kukamilisha kazi kwa wakati", amesisitiza Prof. Mbarawa.

Naye mkuu wa wilaya ya Uvinza Dinah Mathamani amesema Wilaya itaendelea kutoa ushirikiano kwa mkandarasi kadri anavyohitaji ili kukamilisha ujenzi huo.

Prof.makame Mbarawa alikuwa katika ziara ya siku tatu kukagua maendeleo ya ujenzi wa miradi ya miundombinu ya barabara na bandari.

Muonekano wa hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa barabara ya Nduta Junction-Kibondo Mjini hadi Kibondo Junction yenye urefu wa kilomita 25 inayojengwa kwa kiwango cha Lami, Wilayani Kibondo, Mkoani Kigoma.



Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa Kampuni ya STECOL Coorporation Limited anayejenga barabara ya Uvinza hadi Maragarasi yenye urefu wa kilomita 51.1 mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wake, Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma. Katikati ni Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) Mkoa wa Kigoma, Mhandisi Naarcis Choma.

PICHA NA WUU
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Bi. Dinnah Mathamani (wa pili kushoto), mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Uvinza hadi Maragarasi yenye urefu wa kilomita 51.1 wakiendelea na ujenzi, Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma.
Mafundi wa Kampuni ya ujenzi ya STECOL Coorporation Limited inayojengwa barabara ya Uvinza hadi Maragarasi yenye urefu wa kilomita 51.1 wakiendelea na ujenzi wa daraja katika barabara hiyo, Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma.


Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) Mkoa wa Kigoma, Mhandisi Narcis Choma (wa pili kulia), wakati alipokagua ujenzi wa barabara ya Nduta Junction-Kibondo Mjini hadi Kibondo Junction yenye urefu wa kilomita 25 inayojengwa kwa kiwango cha Lami, Wlayani Kibondo, Mkoani Kigoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...