Katibu Mkuu Sekta ya Uchukuzi, Gabriel Migire (kulia) akisaini mkataba wa makubaliano  na Katibu Mkuu wa Wizara ya Usafirishaji wa umma kutoka Malawi Hasting Chiudzu, kuhusu mashirikiano katika usafiri wa njia ya Barabara, huduma za bandari katika ziwa Nyasa na uhudumiaji wa mizigo ya Malawi kupitia bandari ya Dar es salaam.

Tanzania na Malawi zimeweka nia ya kushirikiana katika Usafiri kwa Njia ya Barabara, huduma za Bandari katika ziwa Nyasa na  Hudumiaji wa mizigo ya Malawi katika Bandari ya Dar es Salaam.

Hayo yamelezwa na Katibu Mkuu  anayesimamia Sekta ya Uchukuzi Gabriel Migire kwenya Mkutano uliowakutanisha  Makatibu wakuu wa sekta ya Uchukuzi toka Tanzania na Malawi lengo la Mkutano huu ni uboresha usafirishaji kwa njia  ya Barabara,

“huduma za Bandari kwa ziwa Nyasa kwakua ziwa hili lipo katika pande Mbili yaani Tanzania na Malawi pia kuendelea kuwashawishi kutumia Bandari ya Dar es Salaam”Alisema Migire.

Kwa Upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Usafirishaji wa Umma kutoka Malawi Hastings Chiudzu amesema kuwa ni muhimu kwa wizara hizi kushirikiana na kuondoa changamoto  mbalimbali za usafirishaji

Pia katibu Mkuu  huyo  amesema ataendelea kuwashawishi wafanyabishara wa Malawi kuendelea kutumia Bandari ya Dar es Salaam kwani Bandari hii ianautaratibu mzuri  wa kushusha na kupakia Mizigo.

Wataalam hao kutoka Malawi walitembelea Ujenzi wa SGR na Bandari ya Dar Es Salaam na kuipongeza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutekeleza  Mradi huo Mkubwa wa Ujenzi wa SGR pamoja na upanuzi wa Bandari.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...