Na Janeth Raphael - MichuziTv - Dodoma

Katika kuhakikisha mchango wa Sekta ya Madini katika pato la Taifa linafikia asilimia kumi au zaidi ifikapo mwaka 2025 kama ilivyofafanuliwa katika dira ya maendeleo ya Taifa, ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020 pamoja na Mpango wa mkakati wa Tume ya madini Kwa mwaka 2019/2020- 2023/2024.

Katika kuhakikisha azima hiyo inafikiwa Tume ya Madini inatarajia kuwa na mikakati ili kuwa na shughuli za Madini ambazo ni endelevu.

Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo ameyabainisha hayo leo jijini Dodoma wakati akitoa mafanikio ya utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Madini Kwa kipindi cha mwaka 2022/2023 na mikakati ya mwaka 2023/2024.

Mhandisi Lwamo amesema Tume ina mkakati wa kuimarisha usimamizi na udhibiti katika maeneo ya uzalishaji wa Madini Ujenzi na Madini ya viwandani kwa kuongeza wakaguzi wasaidizi wa Madini Ujenzi (AMAs), vitendea kazi (PoS) pamoja na kushirikisha Mamlaka nyingine Serikali zunazosimamia rasilimali hizo. (Halimashauri, Polisi, TARURA NA TANRIROADS).

Mhandisi Lwamo ameedelea kusema kuwa mikakati mingine ni kuimarisha udhibiti wa biashara haramu ya Madini hususani utoroshaji wa Madini Kwa kuhamasisha umuhimu wa kutumia msoko na vituo vya madini nchini, kuimarisha vituo vya ukagizi (ext-points) katika maeneo ya mipakani, bandarini, uboreshaji na usimamizi thabiti wa mfumo wa utoaji wa leseni za madini pamoja na viwanja vya ndege.

Kuimarisha Mazingira ya Uwezeshaji Kwa wachimbaji wakubwa na wachimbaji wa kati wa madini, kuhamasisha shughuli za utafutaji wa Madini Kwa kuendelea kutoa leseni za utafutaji wa Madini nchini.

Aidha Mhandisi Lwamo amesema pamoja na mafanikio makubwa ya Sekta ya Madini yaliyopatikana kutokana na kuanzishwa kwa Tume ya madini pia kuna changamoto zilizojitokeza ambapo ni uelewa mdogo Sheria ya Madini sura ya 123 na kanuni zake kwa wachimbaji na wafanyabiashara wa Madini na Umma kwa ujumla hivyo kusababisha uwepo wa migogoro ya mara kwa mara.

Hata hivyo Sekta ya Madini ni miongoni mwa Sekta muhimu katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya kijamii na Taifa kwa ujumla.

"Mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha Serikali ya awamu ya sita katika Sekta hii yametokana vna uongozi imara wa Rais Samia Suluhu Hassan" - Amesema Mhandisi Lwamo.

Kaimu Katibu Mtendaji WA TUME ya Madini Mhandisi Ramadhani Lwamo akizungumza na wanahabari kuelezea mafanikio ya utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Madini kwa Kipindi cha mwaka 2022/2023 na mikakati ya mwaka 2023/2024. 




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...