Na Grace Semfuko, MAELEZO.

Tanzania ni mojawapo ya Nchi Mwanachama wa Umoja wa Afrika zilizoridhia mpango wa hiari wa Afrika wa kujitathmini kiutawala Bora APRM


Mfumo wa Mapitio ya Vijana wa Afrika (APRM) ulianzishwa mwaka 2002, na mwaka 2003 ulianzishwa na Umoja wa Afrika katika mfumo wa utekelezaji wa Ushirikiano Mpya wa Maendeleo ya Afrika (NEPAD).

APRM ni chombo cha kubadilishana uzoefu, kuimarisha mbinu bora, kutambua mapungufu, na kutathmini mahitaji ya kujenga uwezo ili kukuza sera, viwango na mazoea ambayo husababisha utulivu wa kisiasa, ukuaji wa juu wa uchumi, maendeleo endelevu na kasi ya ushirikiano wa kiuchumi wa kanda na bara.

Nchi wanachama ndani ya APRM zinafanya ufuatiliaji wa kibinafsi katika nyanja zote za utawala wao na maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Wadau wa Umoja wa Afrika (AU) wanashiriki katika kujitathmini wenyewe kwa matawi yote ya serikali - kiutendaji, sheria na mahakama pamoja na sekta ya kibinafsi, mashirika ya kiraia na vyombo vya habari.

Mchakato wa Mapitio ya APRM unazipa nchi wanachama nafasi ya mazungumzo ya kitaifa kuhusu utawala na viashiria vya kijamii na kiuchumi na fursa ya kujenga maelewano kuhusu njia ya kusonga mbele.

Mpango wa APRM uliwezesha nchi mbalimbali Barani Afrika kuandaa na kutoa ripoti za nchi hizo kwa mara ya kwanza mwaka 2003 ambapo Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizotoa ripoti hizo na kuonesha kufanya vizuri katika suala la Utawala bora na wa kidemokrasia.


Kwa mara nyingine tena Serikali ya Tanzania imekubali kuandaa ripoti ya pili ya mapitio ya nchi ya Mpango wa hiari wa Afrika wa kujitathmini kiutawala Bora APRM lengo likiwa kujitathmini ilikotoka na mwelekeo wa sasa katika kusimamia utawala bora na wa kidemokrasia, siasa safi, usimamizi wa uchumi, uendeshaji wa mashirika ya biashara na utoaji wa huduma za kijamii.

Katika mchakato wa maandalizi wa ripoti hiyo, Tanzania imetembelewa na Uongozi wa juu wa Bara la Afrika wa APRM ambapo kwa pamoja wamejadili mikakati ya kuimarisha ripoti hizo huku Tanzania ikipongezwa kwa juhudi zake za kuimarisha utawala bora.

Akizungumza Agosti 05, 2023 katika Mkutano kuhusu uhauishaji wa APRM Tanzania na maandalizi ya ripoti ya pili ya tathmini ya Utawala Bora Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balizi Fatma Rajab amesema uamuzi wa Serikali ya Tanzania ni wa kupongezwa.

“Tumekutana leo hii ili kuwakaribisha wageni wetu kutoka Bara wa APRM kufuatia uamuzi wa Serikali yetu kukubali nchi yetu kuandaa ripoti ya pili ya mapitio ya nchi ya APRM huu ni uamuzi mzuri sana unaopaswa kupongezwa, tangu nchi yetu iandae ripoti ya kwanza mwaka 2013, mambo mengi yamebadilika, tumeshuhudia mabadiliko ya viongozi mbalimbali masuala mbalimbali yametokea pamoja na vipaumbele vya Serikali na jamii zetu kubadilika kwa ujumla, lengo letu kama Serikali ni kutaka kujitathmini kuona tumetoka wapi, tupo wapi na tunafanyaje ili kuendelea kusonga mbele kwa kusimamia utawala bora hususan masuala ya demokrasia na siasa usimamizi wa uchumi, uendeshaji wa mashirika ya biashara, na utoaji wa huduma za kijamii.” Amesema Balozi Fatma Rajab.


Bi Rajab amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amekubali kuandaa ripoti ya pili ya mapitio ya nchi ya APRM, ambapo ripoti ya kwanza ilifanyika mwaka 2003.

“Rais amekubali kuandaa ripoti ya pili ya mapitio ya nchi ya APRM, ripoti ya kwanza ilifanyika mwaka 2003, tumepokea taarifa ya ujio wa ujumbe APRM ngazi ya Bara la Afrika ambao wanatokea nchini Afrika Kusini ambako ndipo kuna Makao Makuu ya Taasisi ya APRM, na inayo matawi katika kila nchi mwanachama wa Umoja wa Afrika zilizoridhia mpango huo, moja ya malengo mahsusi ya ziara hiyo ni kukutana na wataalamu wabobezi kujadiliana kuhusu maandalizi ya ripoti ya pili ya tathmini ya utawala bora nchini” amesema Balozi Fatma Rajab.

Nae Mtendaji Mkuu wa mpango wa hiyari wa Afrika wa kiujitathmini katika Demokrasia na Utawala Bora APRM Profesa Edward Maloka amesema ripoti ya pili ya kujitathmini kiutawala bora kwa nchi za Afrika utasaidia katika kuleta uwazi Pamoja na uelekeo wa nchi hizo ambapo tangu kuanzishwa kwa mpango huo miaka 20 iliyopita Afrika imeshuhudia nchi nyingi kujiendesha kwa uwazi na kidemokrasia.

“Sisi APRM tunasherehekea miaka 20 tangu kuanzishwa kwa taasisi hii, tunaposherehekea miaka hii tunashiriki kikamilifu katika mazingira ya Tanzania na mafanikio yake katika utawala bora na wa kidemokrasia, Sekretariet ya APRM Bara la Afrika na Baraza la Taifa la Usimamizi wa APRM tutahakikisha tunakwenda sawa kwenye mipango ya nchi na mikakati yao.” Amesema Profesa Maloka.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa APRM Tanzania Profesa Hasa Mlawa amesema ujio wa ugeni huo kutoka APRM Makao Makuu nchini Afrika Kusini umekuwa na mafanikio makubwa katika maandalizi ya ripoti ya pili ya APRM.


“Tumepokea taarifa ya ujio wa ujumbe APRM ngazi ya Bara kutoka nchini Afrika Kusini ambako ndipo makao makuu ya Taasisi ya APRM na inayo matawi katika kila nchi mwanachama wa Umoja wa Afrika zilizoridhia mpango huo, moja ya malengo mahsusi ya ziara hiyo ni kukutana na wataalamu wabobezi kujadiliana kuhusu maandalizi ya ripoti ya pili ya tathmini ya utawala bora nchini.” Amesema Profesa Mlawa.

Jukwaa la Wakuu wa Nchi na Serikali wa APRM lilipitisha Mpango Mkakati wa 2016-2020 na Mkataba wa APRM katika Mkutano wa 25 wa Kilele wa Jukwaa la APRM uliofanyika Nairobi , Kenya. Bunge la 28 la Wakuu wa Nchi na Serikali wa AU liliongeza zaidi mamlaka ya APRM kujumuisha ufuatiliaji wa utekelezaji na kusimamia mipango muhimu ya utawala ya Bara. Aidha, Bunge la AU liliongeza muda wa majukumu ya APRM kujumuisha ufuatiliaji wa utekelezaji wa Ajenda 2063 ya Umoja wa Afrika (AU) na Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs), Agenda 2030.


Mnamo 2018, Mkutano wa 11 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa AU ulifikia uamuzi wa kuunganisha kikamilifu APRM kwenye Umoja wa Afrika kwa mujibu wa uamuzi wa Bunge uliopitishwa na Mkutano wa 28 wa Kawaida wa Umoja wa Mabunge uliofanyika. mjini Addis Ababa.

Bunge lilihimiza zaidi kujiunga kwa jumla kwa nchi wanachama wa AU kwenye APRM, ambayo sasa inahesabu wanachama 40 kwa kujiunga na Jamhuri ya Shelisheli na Zimbabwe katika Kongamano la 32 la APRM Mjini Addis Ababa, Ethiopia, Januari 2020.


Mpango wa APRM unaangazia maeneo makubwa manne yakiwepo ya demokrasia na utawala bora wa kisiasa, utawala na usimamizi wa kiuchumi, utawala bora na maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi.





Picha mbalimbali zikionesha wadau wa Mpango wa Hiari wa Afrika wa Kujitathmini Kiutawala Bora wakiwa katika majadiliano ya mchakato wa kuandaa ripoti ya pili inayotarajia kuwasilishwa mwakani, majadiliano hayo pia yaliwashirikisha viongozi wa juu wa APRM Bara la Afrika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...