NA
K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
MKURUGENZI
Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSF), CPA. Hosea
Kashimba amesema uwekezaji uliofanywa na PSSSF kwenye eneo la viwanda vya
kuongeza thamani ya bidhaa za kilimo na mifugo unaenda kuongeza nguvu moja kwa
moja wazo la Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania la kuongeza ushiriki wa vijana kwenye kilimo chini ya mpango wa
Building a Better Tomorrow (BBT)
CPA.
Kashimba ameyasema hayo kwenye banda la PSSSF kwenye Maonesho ya Kimataifa ya
Kilimo Tanzania kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya Agosti 7, 2023,
ambapo Mfuko unatoa huduma kwa wanachama na wastaafu lakini pia elimu kuhusu
fursa mbalimbali zilizopo ikiwemo uwekezaji.
Alisema juhudi za Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuleta mapinduzi kwenye sekta ya kilimo nchini zinapaswa kuungwa mkono na watanzania wote na PSSSF iko tayari kuhakikisha vijana wa kitanzania watakaoingia kwenye sekta ya kilimo wanafaidika.
Alisema
PSSSF tayari imewekeza kwenye kiwanda cha kuchakata tangawizi kilichoko Mamba
Miamba wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, kiwanda cha Chai Mponde kilichoko
wilaya ya Lushoto, mkoani Tanga, lakini pia kuna viwanda vya kuonegza thamani mazao
yatokanayo na mifugo kama vile machinjio ya kisasa Nguru, wilaya ya Mvomero
mkoani Morogoro na kiwanda cha bidhaa za ngozi kilichoko Kilimanjaro.
Mradi wa Building a Better Tomorrow (BBT) unaolenga kuongeza ushiriki wa vijana katika kilimo
kwa kuwapatia mafunzo, maeneo ya mashamba, mitaji na kuwaunganisha na fursa za
masoko ulilizinduliwa Agosti 2022 na tayari kundi la kwanza la vijana wapatao
800 wamehitimu mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kuendesha kilimo biashara.
“Vijana hawa watakapokuwa wanaanza shughuli za
uzalishaji, ufugaji na kilimo wanakuwa na uhakika wa kuuza mazao hayo, viwanda
vyetu vitapokea tanagawizi, tutapokea mifugo iliyonenepeshwa na bidhaa nyingine
zinazoendana na viwanda tulivyowekeza.” Alifafanua CPA. Kashimba.
Kuhusu
ushiriki wa Mfuko kwenye Maonseho hayo ya Nanenane, CPA Kashimba alisema pamoja
na kuwahudumia wananchama na wananchi kwenye banda la Mfuko huo, pia wafanyakazi
wa PSSSF wakiongozwa na nyeye binafasi wameendelea na kampeni ya ‘Banda kwa
banda’ kwa kuwatembeela wanachama kwenye mabanda yao na kusikiliza maoni yao lakini
pia kutoa elimu ya matumizi ya huduma za PSSSF Kiganjani ambayo haimuhitaji
Mwnachama kufika kwenye ofisi za PSSSF ili kuhudumiwa.
“Tunatambua
wanachama wa PSSSF, ni watumishi wote wa serikali kuu, serikali za mitaa na
mashirika ambayo serikali ina umiliki wa hisa zaidi ya asilimia 30%, wanachama
hawa nao wako hapa kuwahudumia wananchi, hivyo tumeona ni busara kwa wale ambao
wamebanwa na majukumu tunawafikia huko waliko na kuwahudumia lakini pia
kuwasikiliza.” Alisema.
Miongoni
mwa mabanda aliyotembekea ni pamoja na BoT, Wizara ya Fedha ambayo imebeba
taasisi zote zilizo chini ya wizara hiyo, Azania Bank, WCF na NSSF.
Maonesho
ya mwaka huu yamebeba kaulimbiu isemayo “Vijana na Wanawake ni Msingi imara wa
Mifumo Endelevu ya Chakula” na yalifunguliwa rasmi Agosti 1, 2023 na Makamu wa
Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango na yanatarajiwa kufungwa Agosi 8, 2023 na
Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mkurugenzi
Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba (wapili kulia) akimkabidhi kijitabu chenye
miongozo mbalimbali ya Mfuko huo, Mkurugenzi wa Usimamizi Rasilimali Watu na
Utawala, BoT, Kened Nyoni wakati alipotembelea banda la BoT kwa nia ya kutoa
elimu na kuwahudumia. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Bodi ya Bima ya Amana,
Isack Kijwili (kulia) na Noves Moses, Meneja Msaidizi Idara ya Mawasiliano
Mkurugenzi
Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba (kushoto) akimkabidhi kijitabu chenye
miongozo mbalimbali ya Mfuko huo, mmoja wa wanachama wa mfuko huo ambaye ni mtumishi wa Wizara ya Fedha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...