Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

WAKALA wa Barabara Vijijini na Mijini(TARURA) umeeleza kwa kina kuhusu Mpango na utekelezaji wa kazi za ujenzi na matengenezo ya miundombinu ya barabara kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Akizungumza leo mbele ya waandishi wa habari Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff wakati akielezea utekelezaji wa majukumu ya wakala huo na muelekeo wake katika mwaka wa fedha 2023/2024 amesema katika mwaka wa fedha 2023/24, jumla ya barabara zenye urefu wa kilometa 21,057.06 zitafanyiwa matengenezo.

Ameongeza kilometa 427 zitajengwa kwa kiwango cha lami, kilometa 8,775.62 zitajengwa kwa kiwango cha changarawe, madaraja na makalavati 855 yatajengwa pamoja na mifereji ya mvua kilometa 70.

Aidha amesema jumla ya Sh bilioni 858.517 zimeidhinishwa kwa ajili ya ujenzi, ukarabati na matengenezo ya miundombinu ya barabara za Wilaya.Kati ya fedha hizo, Sh.bilioni 710.31 ni fedha za ndani na Sh. bilioni 148.207 ni fedha za nje kupitia miradi ya RISE, TACTIC, Bonde la mto Msimbazi na Mradi wa Agri connect.

"Mojawapo ya kipaumbele cha TARURA ni kutumia malighafi zinazopatikana maeneo ya kazi ili kupata ufanisi wa gharama za ujenzi. Hadi Mwezi Machi, 2023 TARURA imejenga madaraja 163 ya mawe yenye thamani ya shilingi bilioni 8.7 ambapo gharama imepungua kwa zaidi ya asilimia 50.

"Madaraja hayo yamejengwa katika mikoa ya Kigoma 92, Singida 24, Tabora 5, Kilimanjaro 10, Mbeya 2, Arusha 6, Morogoro 2, Rukwa 3, Pwani 1, Ruvuma 3 na Iringa 15, " amesema.

Pia amesema wanaendelea kufanya majaribio ya teknolojia mbalimbali ili kutumia udongo uliopo eneo la kazi badala ya kusomba kutoka maeneo mengine ya mbali. Teknolojia hizo ni pamoja na ECOROADS, Ecozyme, na
GeoPolymer.

Amesema hadi sasa kwa kutumia teknolojia ya ECOROADS, katika Jiji la Dodoma imejengwa kilometa 1 ambayo imekamilika na katika Wilaya ya Mufindi zitajengwa km 10 na Mkandarasi yuko kwenye matayarisho ya kuanza kazi.

Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema Watanzania wana kila sababu ya kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa dhamira yake ya kuhakikisha taasisi zote za Serikali zinazofanya biashara na zisizofanya biashara zinafanya kazi zake kwa tija.

"TARURA imeanzishwa mwaka 2017 lengo likiwa ni kupanua mawanda ya namna ambavyo tutawahudumia Watanzania kwa kuwaboreshea barabara."



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...