Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amawataka wajasiriamali kurasimisha biashara zao ili waweze kufanya biashara kwa wigo mpana zaidi.

 Dkt. Gwajima ameyasema hayo  tarehe 24 Agosti, 2023 katika ufunguzi wa Kongamano la Wanawake na Ununuzi wa Umma lililoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Ng'arisha Maisha Foundation Jijini Tanga, lenye lengo la kutoa mwamko kwa wajasiriamali ili waweze kuchangamkia fursa mbalimbali zinazopatikana baada ya kurasimisha biashara zao.

Ameongeza kuwa ili kwenda na wakati na kupata fursa zinazotokea katika mchakato mzima wa ununuzi ni vyema wajasiriamali wakarasimisha biashara zao ili kuwa miongoni mwa watakaopata zabuni.

"Natambua kuwa mmekuwa mkiandaa bidhaa bora na wengine mkiwa na huduma ambazo kwa namna moja au nyingine mnapaswa kupata zabuni ila pasipo kurasimisha biashara zenu BRELA na taasisi nyingine itakuwa ni vigumu kupata nafasi hizi, hivyo mfike kurasimisha biashara zenu", amesema Dkt. Gwajima.

Kwa upande wake Afisa Usajili kutoka BRELA Bw.Abdul Songolo akifafanua kuhusu huduma zinazotolewa na na Taasisi katika Kongamano hilo amesisitiza kuwa milango ya kufungua biashara ipo wazi na BRELA imerahishisha huduma kwani wanaweza kujisajili mahali popote walipo kupitia mfumo wa Usajili kwa njia ya Mtandao (ORS).

Amesisitiza  kuwa BRELA inaendelea kuwasogezea wadau huduma ikiwa ni pamoja na kuwafikia mahali popote ili kutoa mafunzo na huduma za papo kwa papo.

Wajasiriamali zaidi ya 1,000 wamehudhuria Kongamano hilo na kuonesha mwitikio mkubwa katika kuchangamkia fursa hasa za kusajili biashara zao.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wanawake na Makundi Maalum Dkt.Dorothy Gwajima akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Wanawake na Ununuzi wa Umma  lililofanyika  jijini Tanga.


Baadhi ya watendaji wa Mkoa na Wizara na Wanawake katika Kongamano lililofanyika Mkoani Tanga

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...