Na Khadija Kalili, Michuzi TV
SHIRIKA lisilo la Kiserikali la Consciousness for Humanity :Utu Kwanza" limeandaa mbio za hisani zitakazofahamika kwa jina la ' Utu Kwanza Run ' kwa ajili ya kuchangisha fedha za kuwasaidia wananchi mbalimbali walio katika nafasi finyu ya kupata huduma ya msaada wa kisheria ikiwemo huduma ya kwanza ya kisheria (first response) hususan kwa wale walioko magerezani na mahakamani pamoja na familia zao.

Akizungumza na vyombo vya habari leo tarehe 10 Septemba, 2023 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Shirika hilo Wakili Shehzada Walli amesema, mbio hizo zinatatajiwa kufanyika Septemba 10, 2023 jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Leaders Kinondoni na kutoa wito wito kwa kila mmoja kuunga mkono Utu Kwanza Run katika kufanikisha mbio hizo.

"Ili kuweza kufanikisha tuliyoazimia kama taasisi ya Utu Kwanza ikiwemo kutoa msaada wa kisheria pamoja na huduma ya kwanza ya kisheria (first response) kuwasaidia wananchi mbalimbali hususan walioko mahakamani, tumeamua kuja na mbio maalum zinazoitwa Utu Kwanza Run kwa lengo la kuchangisha fedha I'll kufanikisha azma hiyo " amesema Wakili Walli na kuongeza

"Utu Kwanza Run itafanyika Septemba 10, 2023 ambapo katika siku hiyo kuanzia saa 4a asubuhi hadi saa 8 mchana kutakuwa na dawati la kutoa msaada wa kisheria hususan wale walioko magerezani. Tunawaomba familia zao waweze kujumuika nasi siku hii."

Wakili Walli amesema, kutakuwa na mbio za kilometa 5 na 10 hadi kilometa 60 kwa wanaokimbia na kutembea, kwa upande wa waendesha baiskeli itakuwa ni kilometa 25 hadi kilometa 60 .

Wakili Walli ameeleza kuwa huduma ya kwanza ya msaada wa kisheria na msaada wa kisheria kwa ujumla watakaoutoa itatolewa kwa kuanzia katika Mahakama ya Mwanzo na Mahakama ya Wilaya na kubainisha kuwa katika mahakama hizo wengi wao wako katika nafasi finyu sana ya kupata msaada wa kisheria.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uchechemuzi na Maboresho kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), amelipongeza shirika hilo kwa kuja na ubunifu katika utoaji wa huduma za msaada wa kisheria ikiwemo kuja na mbinu tofauti.

"Kitu wanachokwenda kukifanya taasisi ya Utu Kwanza kutoa huduma ya kwanza ya msaada wa kisheria ni cha kipekee na cha kupongeza, kitu ambacho ni tofauti na wadau wengine wanaotoa msaada wa kisheria kwani wamewekeza katika makosa ya jinai, na jambo hili limekuja katika muda mwafaka wa mabadiliko ya mfumo wa haki jinai" amesema Wakili Fulgence Masawe

Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Moil Allif Mansoor amesema, hatua ya taasisi ya Utu Kwanza kuanzisha mradi wa Dawati la Msaada wa Kisheria (Legal Aid Desk Project) inalenga katika kuhakikisha utu na haki ya mtu inapatikana na ni miongoni mwa jambo muhimu sana kwa nchi.

"Tunahitajika kuunga mkono hatua za kupatikana haki na utu, kwa kuwa bila kuhudumia jamii sidhani kama maisha yatakuwa yana maana, tuihudumie jamii ili kuyapa thamani na maana maisha yetu"

Naye Mwenyekiti wa Klabu ya Baiskeli ya Twende Butiama, Gabriel Landa amethibitisha klabu yake kushiriki katika mbio hizo lengo likiwa ni kuhamasisha na kuunga mkono utoaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa watu wanaokosa huduma hiyo na kuongeza kuwa jambo hilo ni la kizalendo.

Consciousness for Humanity pia inajulikana kama "Utu Kwanza" ni Shirika Lisilo la Kiserikali (NGO) lililosajiliwa chini ya Sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. NGO ilianza shughuli zake mwaka wa 2019 na inafanya kazi katika kutafuta kuhifadhi utu na heshima ya binadamu kwa kusaidia hasa wafungwa wote wawili, waliohukumiwa na wasio na hatia, pamoja na familia zao. Dhamira ya shirika hili ni kutetea utu kwa kuimarisha ubora wa maisha ya jumuiya na kutoa uhakikisho kupitia usalama na uthabiti.

Washiriki na wachangiaji wanaweza kutuma pesa za kuchangia kwa kupitia Lipa Namba ya malipo ya washiriki kuwa ni 5890079 jina Utu kwanza.
Mkurugenzi Mtendaji  wa Kampuni ya Moil Ally Mansoor ametoa wito kwa wafanya biashara wenzake kujitokeza kwa  wingi  kwenye Utu Kwanza Fun run.
Mwenyekiti wa klabu  ya Baiskeli  ya Twende Butiama  Gabriel Landa amesema wanachama wake  watashiriki kwenye  Utu Kwanza Fun Run.
Mkurugenzi Mtendaji  wa Kampuni ya Moil Allif  Mansoor ametoa wito kwa wafanya biashara wenzake kujitokeza kwa  wingi  kwenye Utu Kwanza Fun run.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...