Na Nasra Ismail ,Geita

WAFANYABIASHARA  katika Mamlaka ya Mji mdogo wa Katoro mkoani Geita wamemtuhumu Ofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) ambapo wamedai amekuwa akitumia lugha ya Kiingereza wakati akiwahudumia hali inayosababisha kutokuwa na maelewano kati yao na TRA.

Tuhuma hizo dhidi ya Ofisa wa TRA zimetolewa na wabunge waliofanya mkutano wa hadhara katika mji huo mdogo na kudai kuwa wafanyabiashara hao wamekuwa wakipitia wakati mgumu wakati wakienda kulipia kodi na kukadiriwa kutokana na kutokuelewa lugha inayozungumzwa na Ofisa huyo.

Mbunge wa Jimbo la Geita Joseph Musukuma amueleza Mkuu wa Mkoa wa Geita Martin Shigela na kwamba hali hiyo imesababisha sintofahamu kwa wafanyabiashara kukadiriwa kodi na ofisi ya TRA Katoro lakini baadae wanaibuka maofisa kutoka Geita na kukanusha makadirio ya mwanzo.

“Tunayo ofisi ndogo ya TRA hapa Katoro, maofisa wanaenda kukadiria kodi wanakubaliana wanaanza  kutoa  kodi wiki mbili baadae wanakuja wengine kutoka Geita wanasema ulikadiriwa kidogo.

"Sasa  nauliza ni halali au ni feki ili tuisubiri ile ya Geita,  hatuwezi kuwa na wahuni ambao wanakadiria  leo na kesho tena wanafanya wengine, " amesema Musukuma.

Kwa upande wake Mbunge  wa Mbogwe Nicodemas Maganga amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Geita kuangalia suala wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama Machinga ambao wapo kwenye soko ambalo halina watu,  hivyo wapelekwe eneo lenye watu ili wafanye biashara zao vizuri.

Wakati huo huo Mbunge wa Geita Mjini Costantine Kanyasu amesema  katika kutekeleza ahadi Serikali inatarajia kujenga shule bora ya wasichana Geita mjini itakayogharimu zaidi yaSh.bilioni 4.1 kwa ajili kuleta maji na tayari mkandarasi  ameanza kazi.

Aidha Mbunge wa Bukombe Dotto Biteko amewaomba wana Katoro  kuacha kusikiliza maneno ya uzushi yanayozungumzwa  na wapinzani  kwani wanatumia uzushi huo kumuangusha Raisi Samia Suluhu Hassani badala ya kumuunga mkono.

“Nataka niwaambie Rais Dk. Samia Suluhu Hassan , mama huyu amefanya kazi kubwa sana, hakuna jambo lolote analotaka zaidi ya kuona Tanzania inabadilika.Inawezekana watu hawaelewi kwasababu ya habari za kusikia,  niwaambie nikiwa shuhuda matendo yake yanamtangaza kuliko anavyosema, "amesema Biteko.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa  wa Geita Martin Shigela amewapongeza wabunge wa mkoa huo kwa kazi kubwa wanaoyifanya ya kuhakikisha maendeleo waliyoyahidi yanaendelea kufanyika.

“Niwahakikishie taka katika mkoa wenye viongozi wazuri, katika mkoa wenye viongozi wanaojituma ni katika mkoa wetu wa Geita , wabunge tunaowaona hapa wana uchungu wa maendeleo ya nchi yetu na wanachukizwa na mtu anayekuja kutaka kuwadanganya wananchi wa Geita, ”amesema  Shigela.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...