Na Nasrah Ismail, Geita

Mbunge wa jimbo la Bukombe mkoani Geita Doto Biteko amewaasa wananchi wa jimbo lake kufanya siasa za amani na kuacha kutukanana kwani kufanya hivyo hakutaweza kuharakisha maendeleo katika wilaya hiyo.

Akizungumza na wananchi wa jimbo la Bukombe alisema hakuna maana ya kujigawa kwa itikadi za vyama kwani jimbo hilo limekaliwa na upinzani pamoja na chama tawala ambapo maendeleo makubwa yameonekana katika utawala wa CCM.

Biteko aliongeza kuwa wakati  wilaya hiyo inatawaliwa na upinzani ilikuwa ya mwisho katika kila eneo ambapo kulikuwa na zahanati tatu na vituo viwili vya afya ,barabara km 256 pekee pamoja na mtandao wa maji kuwa chini ya asilimia 15%;

“leo hii tumetoka kwenye zahanati 3 wilaya nzima lakini sasa tuna zahanati 11 ambazo tumejenga wenyewe, tuna maboma mapya ya zahanati 24, leo hii tuna vituo vya afya 7 kwenye wilaya yetu na pia tutapandisha hadhi kituo cha afya cha Uyovu kuwa hospitali ili watu wa ukanda huu wasiwe na sababu ya kwenda Ushirombo kwa ajili ya kufata huduma za afya.” Alisema Biteko.

Aidha Biteko aliongeza kuwa hospital ya wiliya ilikuwa na hadhi kama zahanati lakini sasa imepandishwa hadhi ikiwa pamoja na kujenga majengo ya dharura,jengo la mama na mottoto pamoja na jingo la wagonjwa mahututi(ICU) kwa ajili ya kuboresha huduma.

“niliahidi kwenye uwanja huu nikawaambia tukichaguana nitatoa leseni kwenye eneo linalozunguka mgodi wa magoti mpaka navyozungynza wapo watu wa uyovu wana leseni pale tumetoa leseni 58 wapo watu wanachimba kule.” Alisema Biteko.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...