Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ameuagiza uongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kuhakikisha mchakato wa kuwapata walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaanzia ngazi ya Kijiji na kisha kupelekwa kwenye Baraza la Kata ili wajiridhishe na hatimaye katika Halmashauri ya Wilaya ili nao wajiridhishe na kuondoa dosari kabla majina hayo hayajawasilishwa TASAF Makao Makuu.

Mhe. Simbachawene ametoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti katika Kata ya Mlunduzi inayoundwa na Vijiji viwili ambavyo ni Chinyika na Chinyanhuku kupitia mikutano yake ya hadhara ya kuelezea utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 katika Jimbo la Kibakwe, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.

Amesema lengo kuu la kubadili mchakato huo wa namna ya kuwapata walengwa ni kumaliza kabisa malalamiko kutoka kwa wananchi wanaodai kuwa mpango huo umekuwa ukiwanufaisha wasio walengwa huku walengwa halisi wakiachwa.

Amesema Serikali ina nia njema katika kuzisaidia kaya masikini, lakini kuna changamoto kubwa inayolalamikiwa na wananchi wengi ikiwemo ya watu wasiohusika kuingizwa kwenye mpango huo ambao hawaendani na malengo ya mpango.

Aidha, Mhe. Simbachawene ameitaka TASAF katika msimu ujao kuangalia namna ya kuwaondoa walengwa ambao wamekidhi vigezo kwa kuwa tayari wamekuwa na uwezo wa kuanzisha miradi inayowawezesha kujikimu kimaisha ili nafasi hizo zichukuliwe na walengwa wenye sifa ambao hawako kwenye mpango na wanakidhi vigezo vya kuingizwa kwenye Mpango huo wa Kunusuru Kaya Masikini.

"Zoezi hili lihusishe walengwa wa TASAF ambao tayari wameweza kujikimu kimaisha kwa kuanzisha miradi ambayo inawawezesha kupata mahitaji yao muhimu ya kimaisha na kukidhi vigezo vya kutokuwa kaya masikini tena,” amesisitiza Mhe. Simbachawene.

Maelekezo ya Mhe. Waziri yanafuatia malalamiko kutoka kwa wananchi kuwa walengwa wanaostahili kuingizwa kwenye mpango wameachwa huku wale wasiostahili ndo wamekuwa wanufaika.



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na wananchi wa Kata ya Mlunduzi kupitia mkutano wa hadhara ya kuelezea utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 katika Jimbo la Kibakwe, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.



Diwani wa Kata Mlunduzi, Mhe. Orgenes John akizungumza wananci wa Kata hiyo kabla ya kumkaribisha Waziri Mhe. George Simbachawene kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara ya kuelezea utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 katika Jimbo la Kibakwe,
Diwani wa Viti Maalum wa Kata ya Rudi, Mhe. Dorisia Fweda akizungumza wananchi wa Kata ya Mlunduzi kabla ya kumkaribisha Waziri Mhe. George Simbachawene kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara ya kuelezea utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 katika Jimbo la Kibakwe,
Mwenyekiti wa Halmashuri ya Wilaya ya Mpwapwa, George Fuime akizungumza wananci wa Kata ya Mlunduzi kabla ya kumkaribisha Waziri Mhe. George Simbachawene kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara ya kuelezea utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 katika Jimbo la Kibakwe,


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...